Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Zanzibar Ali Haji Hassan akifunguwa Mafunzo ya Amani na maendeleo kwa Vijana kutoka Taasisi mbali mbali za Serikali na Binafsi kutoka Zanzibar huko katika Kituo cha elimu Mbadala Rahaleo.
Mkoa wa Mjini Magharibi.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Zanzibar Ali Haji Hassan amewataka Vijana kuwa Wazalendo kwa kudumisha Amani na Utulivu ili kuimarisha maendeleo ya nchini.
Ameyasema hayo katika Kituo cha Elimu Mbadala Rahaleo wakati alipokuwa akifunguwa Mafunzo ya Amani na maendeleo kwa Vijana kutoka Taasisi mbali mbali za Serikali na Binafsi Zanzibar.
Amesema Mashirikiano na Amani, yanapelekea kuleta maendeleo na kutoa fursa mbalimbali za kiuchumi.
Aidha amesema Amani ni chachu ya maendeleo kwani inatoa fursa nzuri ya kutekelezwa Miradi ya Maendeleo, itakayoweza kuzalisha ajira kwa Vijana.
Amefahamisha kuwa, baadhi ya Vijana wanavipaji vikubwa hivyo wanahitaji kuhamasishwa na wengine ili waweze kuwajengea uwezo wa kuzifikia fursa zilizopo.
Amesema Baraza la Vijana linaendelea na mkakati wa kuimarisha mashirikiano kwa Taasisi mbali mbali za Vijana ikiwemo wenye mahitaji maalumu na Wanawake.
Nae Mkurugenzi wa Center for Youth Dialogue (CYD) Hashim Salum Pondeza amelipongeza Baraza la Vijana Taifa kwa juhudi kubwa wanazozichukuwa za kuwaunganisha pamoja Vijana kutoka sekta zote na kuangalia uwezekano wa kuwasaidia kulingana na mahitaji yao.
Kwa upande wake Afisa Mawasiliano na Program kutoka CYD Joeilbert Shamte amesema azimio la Umoja wa Mataifa, nambari 2250 inasisitiza suala la Vijana, Amani na Usalama wao.
Nao Vijana walioshiriki katika mafunzo hayo wamesema ukiukwaji wa sheria ni moja kati ya sababu zinazoweza kusababisha Uvunjifu wa Amani hapa Nchini.
Aidha wameiyomba Serikali kuweza kudhibiti Uingiaji na utokaji wa watu ili kunusuru kusababisha kufanyika kwa vitendo vya uvunjifu wa Amani,ikiwemo Vitendo vya Udhalilishaji uporaji pamoja na Utumiaji wa Dawa za kulevya.
Hata hivyo Vijana hao wamesema wanahitaji kujengewa uwezo kwa kupatiwa Mafunzo ya stadi za maisha ili waweze kujielewa na kufahamu haki zao za msingi sambamba na kupatiwa Ufumbuzi Changamoto zinazowakabili.
Mbali na hayo wameomba kurejeshwa malezi ya pamoja na Vijana kupatiwa mafunzo ya maadili ili waweze kuwa raia wema wa kuijenga Nchi yao.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Zanzibar Ali Haji Hassan akifunguwa Mafunzo ya Amani na maendeleo kwa Vijana kutoka Taasisi mbali mbali za Serikali na Binafsi kutoka Zanzibar huko katika Kituo cha elimu Mbadala Rahaleo.
Mkurugenzi wa Center for Youth Dialogue (CYD) Hashim Salum Pondeza akitoa maelezo katika Mafunzo ya Amani na Maendeleo kwa Vijana katika Kituo cha elimu Mbadala Rahalaeo.
Afisa Mawasiliano na Program kutoka CYD Joeilbert Shamte akiwasilisha mada kwa Vijana juu ya Amani na Usalama katika Kituo cha Elimu Mbadala Rahaleo.
Baadhi ya Vijana kutoka Taasisi za Serikali na Binafsi Zanzibar wakimsikiliza kwa makini, Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Zanzibar Ali Haji Hassan (hayupo pichani) wakati alipokuwa akifunguwa Mafunzo ya Amani na maendeleo ya Vijana huko Kituo Cha Elimu Mbadala Rahalaeo.