Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .MAMLAKA ya hifadhi ya Ngorongoro imezindua kampeni ya msimu wa sikukuu Ngorongoro “Merry and Wild Ngorongoro Awaits ” inayotarajiwa kuanza desemba leo hadi januari 4 ,2025 katika kuelekea msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka 2024.
Aidha kampeni hiyo inaenda na kauli mbiu isemayo “Merry and Wild; Ngorongoro Awaits” ambapo katika utekelezaji wa kampeni hii NCAA itashirikiana na kampuni ya Smile Safaris ya Jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari,Kamishna msaidizi mwandamizi idara ya utalii na masoko , Mariam Kobelo amesema mamlaka ya Ngorongoro imeamua kuanzisha kampeni hiyo kwa mwaka huu kuweza kuongeza idadi ya watalii wa ndani na kuwezesha watanzania kuwa sehemu ya kufahamu vivutio vilivyopo katika hifadhi hiyo.
Aidha amesema kuwa,katika msimu wote wa kampeni hii ya mwezi mmoja kampuni ya Smile Safaris kwa kushirikiana na NCAA imeandaa vifurushi (package) vilivyogawanyika katika makundi matatu kama ifuatavyo;
Kifurushi cha kwanza kinaitwa Faru ambacho gharama yake kwa kila mtu ni Shilingi 450,000 ambapo watakaolipia kifurushi hiki watafanya utalii kwa siku mbili (02) na gharama hizo zitajumuisha kiingilio, Malazi, Chakula, muongoza watalii, Usafiri na huduma ya picha ambapo watakaolipia kifurushi hiki safari ya Ngorongoro itafanyika tarehe 24-25 Desembaa 2024.
Kifurushi cha Pili kinaitwa Tembo ambayo gharama yake kwa kila mtu itakuwa Shilingi 130,000 wahusika watafanya utalii kwa siku moja (01) Day trip na gharama hizo zitajumuisha kiingilio, Chakula, muongoza watalii, Usafiri na huduma ya picha.
Kifurushi cha tatu kinaitwa Chui ambayo gharama yake kwa kila mtu itakuwa Shilingi 85,000 wahusika watafanya utalii kwa siku moja (01) na gharama hizo zitajumuisha Usafiri wa basi, kiingilio, Chakula, muongoza watalii na huduma ya picha.
“Katika utekelezaji wa Kampeni hii pamoja na kutangazia umma kupitia mkutano huu wa vyombo vya habari pia tutatumia vijana maalumu wajulikanao kama Action Rollers Skates ambao watakuwa katika mitaa mbalimbali katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Zanzibar kuanzia tarehe 4 hadi 16 Desemba, 2024.”amesema
Ameongeza kuwa ,katika utekelezaji wa kampeni hii wananchi wote wanakaribishwa na wanaweza kuchagua kifurushi chochote kati ya vitatu tulivyotangaza kwa kupiga namba za simu 0755 559013 kwa ajili ya kuweka booking kupitia kampuni ya Smile Safaris na kupata ufafanuzi na maelezo zaidi.
“Tunawashukuru waandishi wote wa Habari na Vyombo vyenu kwa kuendelea kuwa wadau muhimu katika shughuli za uhifadhi na utalii katika eneo la Ngorongoro na tunaendelea kuwasisitiza kutuunga mkono katika kutangaza kampeni hii.”amesema
Amesema kuwa idadi ya watalii wa ndani wanaotembelea eneo la hifadhi hiyo ni ndogo kulinganisha na wageni wanaokuja kutoka Mataifa mbalimbali duniani hali iliyopelekea kuona umuhimu wa kuwezesha watanzania kutembelea maeneo hayo yanayosimamiwa na hifadhi hiyo.
“Takwimu hii inaonyesha wazi kuwa mwamko wa watanzania kutembelea maeneo ya hifadhi bado ndogo na hivyo kuhitajika msukumo wa sisi kama mamlaka kufanya jitihada za makusudi za uhamasishaji wa wananchi”amesema
Amezitaja fursa za watanzania watakazozipata wakati wakiwa katika eneo la hifadhi hiyo ni pamoja na kutembelea kreta ya Ngorongoro,Kreta ya Empakai na Olmoti,Msitu wa nyanda za juu kaskazini ambao ni makazi ya wanyama wengi ikiwemo ikiwemo Simba,Tembo,Faru,Nyati na Chui.
“Tunawashukuru waandishi wote wa Habari na Vyombo vyenu kwa kuendelea kuwa wadau muhimu katika shughuli za uhifadhi na utalii katika eneo la Ngorongoro na tunaendelea kuwasisitiza kutuunga mkono katika kutangaza kampeni hii.”amesema
Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Tawala mkoa wa Arusha , Daniel Loiruki amesema kuwa,Mkoa wa Arusha upo tayari kushirikiana na Mamlaka katika kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo hifadhi.