Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme (katikati) akiwa katika mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Hasara na Upotevu unaosababishwa na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi Bw. Ibrahima Cheikh Diong (kushoto) leo Novemba 04, 2024 jijini Manila nchini Ufilipino. Kulia ni Mkurugenzi wa Ufuatiliaji nma Tathmini Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sigsbert Kavishe.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme (katikati) akimkabidhi mapendekezo ya maandiko ya miradi mitatu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Hasara na Upotevu unaosababishwa na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi Bw. Ibrahima Cheikh Diong (kushoto) leo Novemba 04, 2024 jijini Manila, nchini Ufilipino. Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) ameambatana na Mkurugenzi wa Tathmini na Ufuatiliaji Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sigsbert Kavishe.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira – (Mazingira) Bi. Christina Mndeme (wa pili toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Hasara na Upotevu unaosababishwa na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi Bw. Ibrahima Cheikh Diong (wa pili toka kulia) Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sigsbert Kavishe (wa kwanza kushoto) pamoja na Msaidizi wa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Hasara na Upotevu Bi. Magret, leo Novemba 04, 2024 jijini Manila, nchini Ufilipino.
……
Tanzania imekabidhi mapendekezo ya maandiko ya mradi 3, kwa ajili ya kuombea fedha kutoka katika Mfuko wa Hasara na Upotevu unaosababishwa na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi.
Hayo yamejiri wakati Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme alipokutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Hasara na Upotevu unaosababishwa na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi Bw. Ibrahima Cheikh Diong Mjini Manila, nchini Ufilipino leo Desemba 04, 2024.
Bi. Mndeme akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Tathmini na Ufuatiliaji Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sigsbert Kavishe wamefanya mazungumzo hayo wakati wa Kikao cha nne cha Bodi ya Mfuko wa Kukabiliana na Hasara na Uharibifu unaosababishwa na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi ambapo Tanzania ni Mwanachama wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabinchi (UNFCCC)
Aidha, katika mazungumzo Bw. Ibrahima ameahidi kufanyia kazi maombi hayo na pia kuipongeza Tanzania kwa kuwa nchi ya kwanza kuwasilisha mapendekezo ya miradi.
Ujumbe wa Tanzania unashiriki katika kikao hicho kinachofanyika kuanzia Desemba 02 hadi 05,2024.