NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Kata ya picha ya ndege Grace Jungulu katika kuhakikisha anaendelea kukijenga na kukiimarisha chama ameahidi kushirikiana bega kwa bega na wenyeviti wote wa mitaa mitatu walioshinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.
Jungulu ameyasema hayo wakati wa kuzungumzia mikakati mbali mbali ambayo amejiwekea mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo na kusema kuwa lengo lake kubwa ni kuendelea kukijenga chama cha mapinduzi kwa kushirikiana na wanachama wengine kuanzia ngazi za mashina na matawi.
Mwenyekiti huyo alisema kwamba ana imani katika kata ya picha ya ndege ataweza kusikiliza kero na changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi kwa kushirikiana kwa hali na mali na wenyeviti wa serikali za mitaa ambao wameweza kuibuka na ushindi kwa lengo la kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
Mwenyekiti huyo alisema kwamba ana imani katika kata ya picha ya ndege ataweza kusikiliza kero na changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi kwa kushirikiana kwa hali na mali na wenyeviti wa serikali za mitaa ambao wameweza kuibuka na ushindi kwa lengo la kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
“Lengo langu kubwa mimi kama mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Picha ya ndege napendakuchukua fursa hii kuwashuru kwa dhati wana chama wote wa ccm ambao wameweza kuwa mstari wa mbele kujitokeza kwa wingi katika zoezi zima la upigaji wa kura na kuweza kushinda katika mitaa yote mitatu hii ni dalili nzuri ya ushirikiano mzuri uliopo katika ya viongozi na wanachama,”alisema Jungulu.
Aidha aliongeza kwamba katika kata ya picha ya ndege amejiwekea mikakati madhubuti ambayo itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo katika sekta mbali mbali ikiwemo, kuboresha miunombinu ya barabara, huduma ya maji safi na salama, afya, elimu, pamoja na huduma nyingine za msingi.
Katika hatua nyingine Jungulu aliwashukuru wanachama wote wa CCM Kata ya picha ya ndege pamoja na wananchi wote kwa ujumla kwa kuweza kufanya maamuzi sahihi na kukiamini chama cha mapinduzi kwa kukipigia kura na kufanikiwa kuweza kushinda kwa kishindo katika mitaa yote mitaa.
Aidha Jungulu alimshukuru Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo ikiwa pamoja na kutenga fedha ambazo zimeweza kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo kuwahudumia wananchi katika nyanja mbali mbali.