NA DENIS MLOWE, IRINGA
Taasisi ya Mtembezi Adventures inayojihusisha kuratibu na kuandaa shughuli mbalimbali zenye lengo la kuhamasisha utalii wa ndani imepanga kutumia Mtembezi Marathon zinazotarajiwa kufanyika Disemba 7 mwaka huu mkoani Iringa kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watanzania.
Akizungumza na wanahabari mjini Iringa katika ukumbi wa Hotel ya Alexander, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mtembezi Adventures, Samson Samwel alisema kuwa mbio hizo zinatarajiwa kushirikisha washiriki zaidi ya 210 waliokishajiandikisha ikiwa na matarajio ya washiriki 500.
Alisema wameamua kuhamasisha utalii wa vivutio mbalimbali vilivyomo mkoani hapa baada ya kubaini katika jamii nyingi kuna dhana kwamba utalii unafanywa na watu wenye kipato kikubwa.
Alisema kuwa harakati za Mtembezi Adventures zilianza tangu akiwa chuo hivyo jamii ielewe kwamba mtu yeyote anaweza kufanya utalii kwa sababu una tija katika maendeleo ya nchi yetu na kukuza kipato.
“Mbio hizi zina lengo kubwa kuhamasisha utalii hivyo tunatamani kuona utalii unakuwa sehemu ya utamaduni wa jamii zetu maana utalii ni moja ya sekta ambazo zinautajiri wa vitu vingi ndani yake ikiwemo miamba”Alisema
Aliongeza kwa kuwashukuru viongozi wa mkoa wa Iringa kwa kumpa ushirikiano mkubwa hali ambayo imempa hamasa kubwa kuelekea kwenye uzinduzi wa mbio hizo ambazo zimekuwa zikifanyika mikoa mbalimbali kuhamasisha utalii.
Alisema kuwa maandalizi ya mbio hizo yamefikia asilimia 94 ya mekamilika na wanatatajia watu wengi kujiandikisha siku ya mwisho na kuwataka watu wajitokezs kuhamasisha utalii.
Amefafanua kwamba kwenye Mtembezi Marathon kutakuwa na mbio za inayoratibu mbio kilometa 21, 10, 5 na 2 na kuwataja baadhi ya wadau waliojitokeza kudhamini mbio hizo kuwa ni Nuru fm radio, Orxy Gas, Alexander hotel , Chagamila general, na 09 liquid Store.
Katika Mbio hizo Samwel alisema kuwa km 2 kwa ajili ya watoto, na zitaanzia Masai Market ambapo km 5 zitaishia Kihesa na km 10 zitaenda hadi Mgongo utofauti mkubwa kati ya marathon zetu na zingine sisi tunafanya kwa ubora zaidi na tuna ujumbe ambao utanufaisha wananchi wa kada mbalimbali na umri tofautitofauti siku hiyo.
“Tumejipanga kuwaalika baadhi ya wasanii na watu mashuhuri kuja kushiriki na sisi kwenye Mtembezi Marathon na kutakuwa na after party itakayofanyika katika lounge ya Royal Tour ambapo msanii Appy atapanda jukwaani.
Kwa upande wake mmoja wadhamini Nuru Fm kupitia mwakilishi wake Emmanuel Goodluck alisema kuwa lengo la kudhamini mbio hizo kuunga mkono juhudi za Mtembezi Adventures katika kukuza utalii mkoa wa Iringa hivyo watu wajitokeza kwa wingi katika mbio hizo.
Alisema Nuru fm itayatangaza mashindano hayo kwa nguvu zote ikiwa lengo ni kuhabarisha umma umuhimu wa utalii kwa nchi yetu hasa Nyanda za Juu Kusini