Mkurugenzi At The Wheel Bw.Amin Lakhani,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha utunzaji wa magari jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo Novemba 30,2024.
Alex Sonna-DODOMA
KAMPUNI ya The Wheel imefungua kituo Cha utoaji huduma za urekebishaji wa haraka na utunzaji wa magari jijini Dodoma Ikiwa ni kituo cha saba Cha kutoa huduma nchini Tanzania.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho, Mkurugenzi At The Wheel Amin Lakhani alisema wamefurahi kupanua huduma hadi Dodoma ambapo lengo ni kuboresha uzoefu wa Uendeshaji Kwa wateja wao.
“Tunafurahi leo kufungua kituo cha kwanza Dodoma ambapo itakuwa ni Cha saba nchini Tanzania.Mtanzamo wetu unahusu ubora,usalama na uamunifu, tukihakikisha Kila safari inakuwa lakini kadri inavyowezekana,”amesema
Ameongeza kuwa:”Kituo hiki kipya kinathibitisha ahadi ya The Wheel kutoa huduma bora wateja, suluhisho sahihi na upatikanaji wa chapa Bora za magari,”
Kwa mujibu wa Lakhani kupitia upanuzi huo wanaendelea kuweka viwango vya ubora katika suluhisho za fitmentza haraka na nafuu.
Alisema kituo hicho kimewekwa vifaa vya kisasa vinavyoendeshwa na mafundi wenye uzoefu ili kuhakikisha usalama wa watu na vyombo vyao.
“Tumeamua kufungua kituo hiki Cha kisasa Kwa kuzingatia Dodoma ndio makao makuu ya Nchi hivyo kitasaidia katika kuhakikisha vyombo vya moto vinakuwa salama,”amesisitiza
Kwa upande wake Afisa habari wa Bluetrain Chris Mendoza alisema ni muhimu watu wakazingatia matengenezo ya vyombo vya moto mara kwa mara Ili kuepusha ajali ambazo zinaweza kuepukika.
Alisema kitaalamu gari unatakiwa kufanyiwa matengenezo pindi inapotembea kilometa 3,000 hadi 5,000 ili vyombo hivyo viwe salama.
Mkurugenzi At The Wheel Bw.Amin Lakhani,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha utunzaji wa nagari jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo Novemba 30,2024.
Mkurugenzi At The Wheel Bw.Amin Lakhani,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha utunzaji wa nagari jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo Novemba 30,2024.