Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 27 Novemba 2024 amepiga Kura ya kuwachagua Viongozi wa Serikali za Mitaa katika Mtaa wa Unyamwezini Kata ya Itumbili, Magu mkoani Mwanza.
Mara baada ya kupiga Kura, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Tax, amesema ameridhishwa na hali iliyopo kituoni hapo na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura ili kutimiza haki ya kikatiba ya kuwachagua viongozi wanaowataka na watakaowaletea maendeleo “Natoa wito kwa Wananchi wenzangu kufika kwenye Vituo vilivyoandaliwa ili waweze kupiga Kura na kutumia haki yetu ya kikatiba na kuwachagua viongozi ambao tunaona tumeridhika nao”
Naye Mkuu wa Wilaya Magu, Mhe. Joshua Nasari amewahakikishia Wananchi Usalama katika vituo vyote wilayani hapo na kuwataka Wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye vituo walipojiandikisha wapate fursa na haki yao kuwachagua Viongozi wa Mitaa, Vitongoji na Vijiji.
Naye Afisa Msimamizi Kata ya Itumbili, Bi. Lina Amata ameeleza kuwa, zoezi la upigaji kura linaendelea vizuri na hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza.