Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mhe. Sharrif Ali Sharrif akimkabidhi tuzo ya Watendaji Wakuu Bora wa mwaka 2024 Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff baada ya kuibuka kinara kwenye Tuzo ya ‘Top 100 Executive List Awards.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Mhandisi Rogatus Mativila na kushoto ni Mwanzilishi wa Kampuni ya Eastern Star Consulting Group Bw. Deogratius Kilawe.
Na. Catherine Sungura – Dar es Salaam
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff amepata tuzo ya utendaji bora na kuwa miongoni mwa Watendaji Wakuu 100, akitambuliwa ni kinara katika tuzo hizo kwa mwaka 2024, katika kategoria ya Mtendaji Mkuu wa mwaka (CEO/MD of the year).
Tuzo hiyo imetolea usiku wa tarehe 24 Novemba,2024 katika ukumbi wa ‘The Super Dome’ Jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mhe. Sharrif Ali Sharrif.
Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo Mhandisi Seff amewashukuru waandaaji wa tuzo hizo, Ofisi ya Rais-TAMISEMI pia watumishi wote wa TARURA na wadau wengine kwa ushirikiano wao katika utendaji wa kazi ambapo imemuwezesha kupata tuzo hiyo.
Tuzo hiyo inayojulikana kama ‘Top 100 Executive List Awards’ huandaliwa na Kampuni ya Eastern star Consulting Group na hii ni mara ya nne kufanyika tangu kuanzishwa nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mhe. Sharrif Ali Sharrif akimpongeza Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff mara baada ya kuibuka kinara kwenye Tuzo ya ‘Top 100 Executive List Awards iliyofanyika kwenye ukumbi wa ‘The super Dome’ jijini Dar es Salaam.
Mtendaji mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff akiongea wakati wa hafla ya tuzo za WatendajiWakurugenzi wakuu 100 wa mwaka 2024.
Picha ya pamoja ya Viongozi mbalimbali wa Makampuni ya Tanzania waliopata tuzo katika kategoria mbalimbali katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya Eastern Star Consulting Group.
Picha ya pamoja ya Mtendaji Mkuu Mhandisi Victor Seff na Menejimenti ya TARURA katika hafla ya tuzo za Watendaji/Wakurugenzi Wakuu 100 wa mwaka 2024.