Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akizungumza wakati akifungua Mafunzo Elekezi ya siku tatu kwa Maofisa Uthibiti ubora wa Wilaya Wateule yanayofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akizungumza wakati akifungua Mafunzo Elekezi ya siku tatu kwa Maofisa Uthibiti ubora wa Wilaya Wateule yanayofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akifafanua jambo wakati akifungua Mafunzo Elekezi ya siku tatu kwa Maofisa Uthibiti ubora wa Wilaya Wateule yanayofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akifafanua jambo wakati akifungua Mafunzo Elekezi ya siku tatu kwa Maofisa Uthibiti ubora wa Wilaya Wateule yanayofanyika jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Bw. Michael John,akielezea lengo la Mafunzo Elekezi ya siku tatu kwa Maofisa Uthibiti ubora wa Wilaya Wateule yanayofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Uthibiti Ubora Wizara ya Elimu,Sayansi na Tekonolojia Bw.Efraim Sembeye,akizungumza wakati wa Mafunzo Elekezi ya siku tatu kwa Maofisa Uthibiti ubora wa Wilaya Wateule yanayofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati akifungua Mafunzo Elekezi ya siku tatu kwa Maofisa Uthibiti ubora wa Wilaya Wateule yanayofanyika jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Mkutano huo, Bw.Antipas Kayombo,akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani) mara baada ya kufungua Mafunzo Elekezi ya siku tatu kwa Maofisa Uthibiti ubora wa Wilaya Wateule yanayofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mafunzo Elekezi ya siku tatu kwa Maofisa Uthibiti ubora wa Wilaya Wateule yanayofanyika jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,amewataka Maafisa Uthibiti ubora wa Wilaya Wateule kwenda kufanya kazi kwa bidii katika kusimamia mageuzi yanayofanywa katika sekta ya elimu kwa sababu wao ni jicho la Wizara.
Prof. Adolf Mkenda,ameyasema hayo leo Novemba 23,2024 wakati akifungua Mafunzo Elekezi ya siku tatu kwa Maofisa Uthibiti ubora wa Wilaya Wateule yanayofanyika jijini Dodoma.
Prof.Mkenda amesema kuwa Rais amewakubali na akakubali muundo wa uwepo wao katika halmashauri zote nchini, akawapa mishahara bora na stahili zao zote katika kutekeleza jukumu hilo la kuthibiti ubora wa elimu nchini.
“Nendeni Mkatupie jicho kwenye tume ya watalaamu kutoka taasisi za elimu nchini ambayo inafanya kazi ya kuiunganisha mifumo ya kuwatambua wanafunzi kuanzia ngazi za elimu ya awali, vyuo vya kati na vyuo vikuu ili ajulikane amesoma wapi, chuo gani na anafanya nini sasa, lengo ni kuwa na mfumo bora wa takwimu za kujua wasomi wake wote nchini.”amesema Prof.Mkenda
Aidha amewataka kutupia jicho mageuzi ya elimu ya msingi ambayo yataanza mwaka 2027 kwa makundi mawili ya wanafunzi yatahitimu shule ya msingi; waliopo darasa la nne watahitimu darasa la saba mwaka huo na waliopo darasa la tatu watahatimu darasa la sita mwaka huo.
Amesema watakapohitimu wataingia kidato cha kwanza ambacho kitakuwa na mikondo mwili; mkondo elimu jumuishi na mkondo wa pili unaohusu elimu ya amali ambayo watajifunza ufundi mbalimbali ukiwemo michezo, muziki, kilimo, uvuvi, ufugaji, na ufundi mwingine.
Hata hivyo Prof.Mkenda amewataka wathibiti ubora hao kwenda kushirikiana na wakurugenzi wa halmashauri na walimu moja kwa moja kwa kuunda kundi la kuwaunganisha kwa ushirikiano huo watatambua changamoto zinazoweza kujitokeza na wajitahidi kutambua shule zote zilizopo katika halmashauri husika.
“Jitahidini kutengeneza mtandao wenu na wakurugenzi na walimu ili muweze kutatua changamoto zinazoweza kujitokeza kwani kuna jambo linaweza kujitokeza na msifahamu ila kwa sababu mmeshatengeneza Mawasiliano mazuri lazima ujue mapema na kulifanyia kazi,” amesisitiza
Prof. Mkenda, amewapongeza wathibiti ubora waliopenya kwenye chekecheke la kuwachuja, kwani hao waliopatikana wamepatikana kwa sifa na vigezo vinavyopimika kwani wana shahada ya uzamili, wana uzoefu na wana maadili na uwezo wa kufanya kazi vizuri.
“Lakini pia niwatia moyo wathibiti ubora 40 waliofeli katika mchujo huo, kwamba waombe kujiendeleza ili wawe na shahada ya uzamili na wizara ipo tayari kuwalipia na wakihitimu wataangaliwa.”amesema
Pia alimwelekeza Mkurugenzi wa Wathibiti Wizara ya hiyo, Ubora Efraim Sembeye kuhakikisha anafanya msawazo wa wathibiti ubora kulingana na ukubwa wa eneo kusitokee eneo ambalo wathibiti ubora wamejazana kuliko eneo jingine na baadhi ya shule zenye walimu wakiume wote ziangaliwe kwani kuna watoto wa kike wanahitaji kusaidiwa na walimu wa Kike.