Mkutano wa 46 wa Baraza la
Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Ngazi ya Wataalam umeanza jijini
Arusha ikiwa ni maandalizi ya Mkutano huo utakaofanyika tarehe 28 Novemba 2024.
Pamoja na mambo mengine,
mkutano wa wataalam unajadili agenda mbalimbali muhimu kuhusu masuala ya
mtangamano wa Jumuiya hiyo ambazo baadaye zitawasilishwa kwenye Mkutano wa
ngazi ya Makatibu Wakuu kwa majadiliano na hatimaye agenda hizo zitawasilishwa
kwenye Mkutano ngazi ya Mawaziri.
Taarifa zilizopokelewa na
kujadiliwa ni pamoja na Taarifa ya utekelezaji wa maamuzi ya awali ya Baraza la
Mawaziri; Taarifa ya Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki;
Taarifa kuhusu masuala Forodha, Biashara na masuala ya kifedha; Taarifa kuhusu
Miundombinu, Sekta za Uzalishaji, Sekta za Kijamii na masuala ya Kisiasa;
Taarifa kuhusu masuala Fedha na Taarifa kuhusu Taasisi za Jumuiya.
Mkutano wa Ngazi ya
Wataalam umeongozwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Tathmini na Ufuatiliaji kutoka
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania, Bw. Haji
Janabi kwa niaba ya Mwenyekiti, Sudan Kusini ambao wameshiriki kwa njia ya
mtandao
Mkutano huu wa ngazi ya
wataalam unafanyika kuanzia tarehe 22 hadi 25 Novemba 2024 ukifuatiwa na
mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 26 Novemba 2024 na tarehe 27 na 28 Novemba 2024 utafanyika
Mkutano wa 46 wa Baraza la Mawaziri ambao utapokea agenda mbalimbali kutoka kwa
Makatibu Wakuu .
Agenda zitakazojadiliwa
katika Baraza la Mawaziri zitawasilishwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi
unaotarajiwa kufanyika tarehe 30 Novemba 2024 kwa ajili ya kupitishwa na
kuridhiwa kwa utekelezaji.
Nchi nane Wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki za Burundi, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo, Rwanda, Somalia, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda zinashiriki mkutano
huo.
Sehemu ya ujumbe wa Burundi wakishiriki Mkutano wa Wataalam |
Ujumbe wa Uganda |
Sehemu ya Wajumbe wakishiriki kikao cha wataalam |
Sehemu nyingine ya wajumbe wakati wa kikao |
Wajumbe wakishiriki kikao |
Ujumbe wa Tanzania wakishiriki kikao |