Njombe, Mbunge wa Lupembe Edwin Swalle amezindua kampeni kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa katika kijiji cha Wanginyi na kisha kuwanadi wagombea wa nafasi ya mwenyekiti ,vitongoji na wajumbe huku akiahidi kwamba endapo watapa ridhaa ya kuongoza atashirikiana nao kutafuta muarobaini wa tatizo la umeme kwa baadhi ya vitongoji,maji,barabara,afya ,kilimo na viwanda vya kuchakata majani ya chai.
Awali akieleza kwanini wananchi wanapaswa kuchagua wagombea kutoka chama tawala CCM Swalle amesema kwasababu chama hicho kimetekelza vyema ilani ya uchaguzi 2020-2025 kwa kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu ,afya ,kilimo na nyingine nyingi ambazo zilikiwa zikipigiwa kelele na upinzani
Kuhusu barabara ya Kibena -Madeke mbunge huyo amesema tayari serikali inakwenda kujenga km 40 kwa kiwango cha lami na kwamba kinachosubiriwa ni kumpata mkandarasi huku pia suala kiwanda cha chai akisema kiwanda cha Ikanga kimetafutiwa muwekezaji.
“Hapa Wanginyi kuna mgombea upinzani hapa ,lakini arudi nyumbani nina kazi ya kumpa kwasababu ni kijana wangu”,alisema Edwin Swalle.
Kwa upande wake Atanas katemba Wanginyi mgombea wa nafasi ya mwenyekiti kijiji akiwa na wagombea wa nafasi ya wenyeviti wa vitongoji amesema kilichomsukuma kugombea nafasi hiyo ni changamoto ya barabara za mitaani,fursa finyu kwa vijana na wanawake elimu na afya.
Katemba amesema endapo atachaguliwa atahakikisha anashirikiana na wananchi pamoja diwani na mbunge kufanya mageuzi ya uchumi na huduma za jamii kijijini hapo hivyo wananchi wamuamini na kukiamini chama chake.
Kwa upande wao wakazi wa wanginyi akiwemo Allen Msanga wanasema wanamtaka kiongozi atakaekuja kumaliza changamoto za akina mama na watoto katika matibabu,elimu ,afya na kuwaunganisha fursa za uchumi.