Baada ya kikao cha Wakuu wa Mamlaka za Mapato za Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki #EARACGs, mjini Nairobi, Kamishna Mkuu TRA Bw. Yusuph Mwenda ametembelea ubalozi wa Tanzania nchini humo na kuwashukuru watumishi wa ubalozini kwa kazi ya uwezeshaji wa shughuli za kibiashara.
Kamishna Mkuu pia amekitembelea kituo cha pamoja cha forodha (Single Customs Territory- SCT) upande wa TRA na kuwataka Watumishi kufanya kazi ya kutathmini bidhaa (valuation) Kwa haraka, umakini na weledi ili kurahisisha biashara Kati ya Tanzania na Kenya.