Na.Alex Sonna,Dar es Salaam
Vigogo wa soka nchini Simba na Yanga wameangukiwa kwa wapinzani wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara,kwenye raudi ya nne ya bora kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba SC watamenyana na Mwadui FC ya Shinyanga na washindi mara nyingi zaidi wa taji la Ligi Kuu, Yanga SC Africans watacheza na Tanzania Prisons timu zote hizo kongwe zitakuwa nyumbani katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mabingwa watetezi, Azam FC watakuwa katika uwanja wao wa Azam Complex kucheza na timu ya Daraja la Kwanza, Friends Rangers ya Dar es salaam.
Upangaji wa ratiba ya Raundi ya Nne ambayo mechi zake zitachezwa kuanzia Januari 24 hadi 26 mwaka, kwa ujumla umehusisha timu 64 za Ligi Kuu, Daraja la Kwanza, Daraja la Pili na zinazoshiriki Ligi za Mikoa.
Ikivuka hatua hiyo, Raundi ya Tano Azam FC itasafiri kumfuata mshindi kati ya Ihefu na Gipco, sawa na Simba ambayo itamfuata mshindi kati ya Maji Maji na Stand United, wakati Yanga itabaki nyumbani kwa ajili ya kucheza na mshindi kati ya Gwambina ya wilayani Missungwi na Ruvu Shooting.
Mechi nyingine za Raundi ya Nne ni Gwambina dhidi ya Ruvu Shooting, African Sports dhidi ya Alliance, Polisi Tanzania dhidi ya Mbeya City, Ndanda FC dhidi ya Dodoma FC, Majimaji FC dhidi ya Stand United, Ihefu FcC dhidi ya Gipco FC na KMC dhidi ya Pan Africans.
Nyingine ni Panama FC na Mtwivila FC, Namungo FC na Biashara United, Mtibwa Sugar na Sahare All Stars, JKT Tanzania na Tukuyu Stars, Kagera Sugar na Might Elephant, Lipuli FC na Kitayosa.
Awali droo hiyo iliyoongozwa na Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Salum Madadi iliuteua Uwanja wa kumbukumbu ya Nelson Mandela mjink Sumbawanga mkoani Rukwa kuwa wenyeji wa Fainali ya michuano hiyo Mei 30, mwaka huu.