MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE)imetoa rai kwa wasanii na wabunifu nchini kubuni logo ya ‘made in Tanzania’ lengo likiwa kutumia logo hiyo kama kitambulisho cha Taifa kwenye bidhaa zinazozalishwa nchini
Akizungumza wakati akizindua shindano hilo leo Novemba 20,2024 Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Latifa Khamis amesema shindano la logo ya ‘Made in Tanzania’ ni muhimu kwa wasanii wa Kitanzania kuonyesha bunifu zao.
Aidha amesema shindano hilo la ubunifu wa logo ya ‘Made in Tanzania’ ambapo kazi za wasanii mbalimbali zitashindanishwa kwa lengo la kupata nembo ambayo itaitambulisha Tanzania katika bidhaa mbalimbali hasa zinasafirishwa nje ya nchi na zile zinazouzwa kwenye masoko ya ndani.
Amesema wasanii na wabunifu nchini wanapaswa kuchangamkia fursa hiyo kwani logo hiyo lengo lake ni kutambulisha bidhaa zenye asili ya Kitanzania katika masoko ya Kimataifa.
“Shindano hili linatoa jukwaa la kipekee kwa wabunifu wa picha na wasanii wa kitanzania katika kuunda utambulisho wa taifa letu na kuonyesha bunifu, fahari, na uwezo ulio ndani ya bidhaa na huduma zetu za ndani.
“Lengo la shindano hili ni kuunda logo inayotambulika na ya kipekee ambayo itakuwa Nembo ya Taifa letu. Logo hii itawakilisha kwa fahari bidhaa na huduma za Tanzania hapa nchini na kimataifa, na kuwa alama ya ubora, imani, na fahari,lengo letu ni kuhakikisha kuwa bidhaa za Tanzania zinafahamika zaidi,”amesema Latifa.
Amesema Tanzania imefanya maendeleo makubwa katika kuongeza mwonekano wake duniani na kuboresha uhusiano wake wa kibiashara kimataifa.
“Licha ya mafanikio yetu mengi,kumekosekana kipengele kimoja,ishara imezindua shindano la ubunifu wa logo ya ‘Made in Tanzania’ ambapo kazi za wasanii mbalimbali zitashindanishwa kwa lengo la kupata nembo ambayo itaitambulisha Tanzania katika bidhaa mbalimbali hasa zinasafirishwa nje ya nchi.a taifa inayounganisha na kuwakilisha ubora na upekee wa bidhaa na huduma za Tanzania katika soko la kimataifa,hapa ndipo shindano la Logo ya Made in Tanzania linapolenga kutoa suluhisho”,Amesema.
Amesema utambulisho wa logo utakuwa utambulisho wenye nguvu wa chapa utaimarisha ushindani wetu, kuongeza mahitaji ya bidhaa na huduma za Tanzania, na kuvutia wawekezaji katika uchumi wetu.
“Nawaalika wabunifu wa picha na wasanii, kutoka mikoa yote ya Tanzania kushiriki katika shindano hili la kihistoria,hii ni nafasi yenu ya kuacha alama ya kudumu kwenye mustakabali wa Taifa,”amesema Latifa.
Amesema kazi zote zinawasilishwa kupitia mfumo wa kigatil kwa kutembelea website ya Tantrade yaani www.tantrade.go.tz ambapo mwisho wa kuwasilisha kazi hizo ni Novemba 24 mwaka na mshiriki ataruhusiwa kukusanya bunifu zisizozidi tatu huku donge nono likihaidiwa kutolewa kwa wabunifu watakaoingia kwenye tatu bora.
Akizungumzia zawadi watakazopata wabunifu hao amesema mshindi wa kwanza atapata Tsh 3,000,000, mshindi wa pili atapata Tsh 2,000,000, na mshindi wa tatu atapata Tsh 1,500,000.