Kaimu Meneja Huduma Ndogo za Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Dickson Gama akizungumza jambo wakati akifungua Mafunzo kwa Wanahabari kuhusu mikopo ya mtandaoni iliyofanyika leo Novemba 14, 2024 jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Huduma Ndogo za Fedha BoT Bi. Mary Ngasa (kushoto) akizungumza jambo wakati akitoa mafunzo kwa wanahabari kuhusu mikopo ya mtandaoni iliyofanyika leo Novemba 14, 2024 jijini Dar es Salaam.
Wanahabari wakiwa katika mafunzo ya kujengewa uwezo kuhusu Mikopo ya Mtandanoni
……..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema itaendelea kutumia rasilimali ili kuhakikisha sekta ndogo ya fedha inakuwa kwa kasi na kuleta tija kwa wananchi kwa kupata huduma bora na kuondokana na umaskini.
Akizungumza leo Novemba 14, 2024 Jijini Dar es Salaam, wakati akifungua mafunzo kwa wanahabari kuhusu mikopo ya mtandaoni, Kaimu Meneja Huduma Ndogo za Fedha BoT, Bw. Dickson Gama amesema kuwa BoT itaendelea kuhakikisha sekta ya fedha inakuwa thabiti, imara na stahimilivu ili kuwawezesha shughuli za uchumi.
Bw. Gama amesema kuwa watahakikisha wanawatambua watoa huduma wote katika sekta ya fedha kwa njia ya mtandao ili kuongeza utulivu.
Amesema kuwa ni jukumu la BoT kusimamia huduma ndogo za fedha nchini, hivyo kwa kutambua umuhimu wa vyombo vya habari wataendelea kuwajengea uwezo ili wawe kiunganishi kati ya benki kuu na jamii kwa ujumla.
“Ukuajiwa wa haraka sekta ndogo ya umesababisha changamoto kadhaa ikiwemo masuala ya kimaadili, riba kubwa, gharama kubwa za mikopo na kukosekana kwa taarifa muhimu” amesema Bw. Gama.
Amesema kuwa licha ya kuwa na changamoto kadhaa wamekuwa mstari wa mbele kutoa elimu ili watoa huduma wafanye kazi kwa na manufaa ya wananchi.
Meneja wa Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Huduma Ndogo za Fedha BoT Bi. Mary Ngasa, amesema kuwa BoT inaendelea kutoa mafunzo ya sheria ya huduma ndogo za fedha pamoja na kanuni zake ili kuwapatia uwezo watoa huduma waweze kuendesha biashara yao kwa ufanisi na kuzingatia haki ya mlaji.
Bi Ngasa amesema kuwa hadi kufika Novemba 2024 wamefanya ukaguzi kwa watoa huduma ndogo za fedha daraja la pili ili kuhakikisha wanazingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.
Amesema kuwa Taasisi 300 zimefanikiwa kukaguliwa, huku taasisi zilizokutwa na mapungufu ya sheria, kanuni na maelekezo ya BoT zimechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kupewa onyo pamoja na kupunguza riba.
Mikopo ya mitandaoni ni mikopo inayotolewa kwa njia ya kidigitali kama vile Applikesheni za simu, tovuti ambayo inapatikana kwa haraka jambo ambalo limeonekana kupendwa na watu wengi, kuongezeka kwa kasi ya mikopo ya mitandaoni imetokana na ukuaji wa teknolojia pamoja na upatikanaji wa haraka wa mikopo ukiwa mahali popote.