Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa anafafanua jambo.
Kaimu mkurugenzi wa Shirika la elimu Kibaha akipanda mti ikiwa ni moja ya ishara kwa ajili ya kuhserekea maadhimisho ya miaka 50 ya shirika hilo tangu lililpoanzishwa.(PICHA NA VICTOR MASANGU).
Baadhi ya viongozi wa serikali pamoja na watumishi wa shirika la elimu wakiwa katika wakiangalia mwenendo mzima wa maandalizi ya siku hiyo (PICHA NA VICTOR MASANGU).
*****************************
VICTOR MASANGU, KIBAHA
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo pamoja na viongozi wengine wa kitaifa kutoka ndani na nje ya nchi kesho wanatarajia kuhudhulia katika kilele cha maadhimisho ya kutimiza miaka 50 ya Shirika la elimu Kibaha ambayo itafanyika katika viwanja vya shirika hilo Wilayani Kibaha.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la elimu Kibaha Robert Shilingi alisema kwamba siku hiyo pia kutafanyika shughuli mbali mbali za kijamii ikiwemo uchangiaji wa damu, upandaji miti pamoja na huduma ya upimaji kwa baadhi ya magonjwa kwa wananchi na watumishi ambayo yatatolewa bila malipo yoyote.
Aidha amebainisha kuwa lengo kubwa la kuanzishwa kwa shirika la elimu Kibaha ni kwa ajili ya kupambana na maadui watatu ambao ni ujunga umasikini pamoja na malazi, sambamba na kuhakikisha inatoa huduma bora katika sekta ya afya pamoja na elimu.
“Siku ya ijumaa januari 10 shirika letu la elimu kibaha litakuwa linatimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake na pia kutakuwa na viongozi mbali mbali wa kitaifa akiwemo Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo pamoja na viongozi wengine ambao watatokea nje ya nchi.
Aidha Shilingi alibainisha kuwa shirika la elimu Kibaha kwa kipindi chote cha miaka 50 limeweza kupata maafanikio makubwa katika Nyanja mbali mbali ikiwemo kuboresha huduma ya matibabu katika hospitali teule ya rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi ambayo imekuwa ikihudumia wagonjwa kutoka maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Pwani na maeneo mengine ya jirani.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa kwa sasa shirika limeweka mipango kabmbe kwa ajili ya kuondokana na changamoto ya chumba cha dharula ambapo wanatarajia kukipanua zaidi lengo ikiwa ni kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wengi ambao wamekuwa wakipata majeruhi wakati wa ajali za barabarani.
“Hospitali teule ya Rufaa ya Tumbi kwa sasa kutokana na kupokea wagonjwa wengine hasa wanaopata ajali za barabarani kutoka maeneo mbali mbali tumejipanga kuboresha zaidi huduma katika chumba cha dharura lengo ikiwa ni kuweza kurahisiha utoaji wa huduma bila ya kuwepo kwa msongamano wa wagonjwa hao,”alisema Shilingi.
Naye mmoja wa wadau wa maendeleo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno amupongeza uongozi wa shirika la elimu Kibaha kwa kuboresha sekta yua afya na elimu na kuwaomba kuendelea kumuenzi hayati Baba wa Taifa hayati Mwalimu juliasi Kambatrage Nyerere katika suala zimala kupamabana na ujinga, umasikini, na malazi.
Pia alisema kuwa Mkoa wa Pwani wananchi wake wengi wamekuwa wakipatiwa matibabu katika hospitali teule ya rufaa ya Tumbi hivyo kunahitajika juhudi za makusidi katika kuboresha miundombinu ya majengo ikiwemo kuongeza vifaa tiba ambavyo vitasaidia kuwapatia matibabu ya uhakika wananchi wake.