Mane mwenye umri wa miaka 27, ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kushika nafasi ya pili mbele ya mchezaji mwenzake wa Liverpool, Mohamed Salah wa Misri miaka ya 2017 na 2018 na kushika nafasi ya tatu mwaka 2016.
Anakuwa mchezaji pekee kutoka Senegal kushinda tuzo hiyo baada ya El Hadji Diouf, aliyeshinda mara mbili, mwaka 2001 na 2002.
Winga wa Senegal, Sadio Mane ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika PICHA ZAIDI SOMA HAPA
Mane ameshinda tuzo hiyo baada ya kura zilizopigwa na makocha wakuu, Wakurugenzi wa Ufundi na Manahodha wa timu za taifa za wakubwa kutoka nchi wanachama wa CAF.
Naye Achraf Hakimi anayecheza kwa mkopo Borussia Dortmund kutoka Real Madrid alishinda tuzo ya Mwanasoka Chipukizi.
Tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka imechukuliwa na Djamel Belmadi baada ya kuiwezesha Algeria kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019.
Nyota wa Ligi Kuu ya England, Serge Aurier wa Totenham, Joel Matip wa Liverpool, kiungo wa zamani wa Everton, Idrissa Gueue, nyota wa Manchester City, Riyad Mahrez na Nahodha wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang wamejumuishwa kwenye Timu ya Mwaka pamoja na Mane na Salah.