Takwimu zinaonesha kuwa kwa mwaka jana, Afrika ilikuwa na chini ya mafunzo elfu kumi ya uthibitisho wa usimamizi wa miradi, ikilinganishwa na Amerika ya Kaskazini yenye zaidi ya elfu 40 na China ambayo iko juu ya laki moja. Hii inaashiria namna ambavyo ujuzi wa usimamizi wa miradi unaweza kuathirika endapo taaluma hii haitazingatiwa kwa uzito.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Allen Manzi, wakati wa kufunga kongamano la kukuza uelewa kuhusu usimamizi wa miradi kwa wataalam. Manzi aliongeza kuwa TCB imepata nafasi ya kuonyesha umuhimu wa usimamizi mzuri wa miradi, jambo ambalo linaweza kuleta thamani halisi katika miradi ya maendeleo.
Aidha, Manzi amesema kuwa kongamano hilo linalenga kuongeza uelewa kwa washiriki na kusaidia kuleta tija katika miradi yote inayotekelezwa na k uhimiza Watanzania kupitia taasisi mbalimbali kuchangamkia fursa ya kujifunza usimamizi wa miradi kama ilivyo kwa nchi nyingine.
Amesema kuwa Tcb imeamua kudhamini kongamano hilo ili kusaidia kuongeza uelewa kwa jamii na pia kuwakumbusha wataalamu ile miiko ya isimamizi wa miradi ili kuhakikisha ile tija ya mradi iliyokusudiwa kwenye kila mradi inapatikana.
“Tcb inatoa wito kwa watu wote walioshiriki kongamano hilo kuhakikisha kwamba yale yaliyozungumzwa katika kongamano yanaongeza ufanisi kwenye utendaji kazi wao na kuongeza uelewa kwa wananchi,lakini pia washiriki hao waweze kuwa mabalozi wa namna ya utumiaji wausimamiaji bora wa miradi ambao utajikita kwenye kuhakikisha kwamba frdha zinazotumika kwenye mradi zinaleta tija iliyokusudiwa na pia maendeleo kwa jamii na nchi kwa ujumla” alisema Manzi
Aidha wataalamu wamebainisha kuwa katika mataifa mengine hii ni fursa ambayo imechangamkiwa kwa kiasi kikubwa na inatumika kuboresha namna ya usimamizi wa miradi,na inafanya miradi yao inakua na tija na ndio maana baadhi ya miradi nchini inasimamiwa na wataalamu kutoka nje ,hii ni nafasiya kupata wataalamu wa kutosha ili waweze kuongeza tija na na ufanisi na ikiwezekana wafike mpaka nje ya nchi kwa ajili ya usimamizi wa miradi
Naye Rais na Mkurugenzi wa Taasisi ya Usimamizi wa Miradi Tanzania, Kheri Mbiro, naye alisisitiza kuwa taaluma ya usimamizi wa miradi inapaswa kuingizwa kwenye mitaala ya elimu kama masomo mengine, jambo ambalo litaleta ufanisi zaidi katika utekelezaji wa miradi.
Aliongeza kuwa miradi inapaswa kufuata muda uliopangwa na kuhakikisha wanafunzi wanapata ujuzi wa kutosha, kwani kushiriki katika mafunzo haya ni njia mojawapo ya kujenga uwezo katika sekta hii.