Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (kushoto ) akizungumza na wafanyakazi wa Baraza la Kiswahili la Taifa (hawapo
pichani) kuhusu kuongeza ubunifu wa miradi ya kusambaza kugha ya Kiswahili katika mifumo ya Tehama leo jijini Da es Salaam alipotembelea ofisi hiyo,Kulia ni Katibu Mtendaji BAKITA Dkt.Selemani Sewangi.
Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa Dkt.Selemani Sewangi (kulia) akitoa ombi kwa Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo
Dkt.Ally Possi (kushoto) la kuomba wizara kuwasaidia fedha za kununua vifaa vya kufundishia ukalimani alipomtelea ofisini kwake na kufanya kikao na wafanyakazi leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (kulia) akipokea zawadi ya Kamusi Kuu ya Kiswahili iliyoandaliwa na Baraza la
Kiswahili la Taifa kutoka kwa Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa Dkt.Selemani Sewangi leo Jijini Dar es Salaam alipotembela ofisi hiyo kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa majukumu.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (kulia) akikagua majengo ya ofisi za Baraza la Kiswahili la Taifa alipotembelea
ofisini hapo leo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa majukumu, kushoto ni Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa Dkt.Selemani Sewangi.
Mfasiri Mkuu wa Baraza la Kiswahili la Taifa Bibi.Vidah Mutasa akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wafanyakazi wenzake kwa Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi mara baada ya kumalizika kwa kikao na kiongozi huyo katika ofisi za baraza leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Baraza la Kiswahili la Taifa alipotembelea ofisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam (watatu kushoto) ni Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa Dkt.Selemani Sewangi.
*********************************
Na Anitha Jonas – WHUSM,Dar es Salaam
02/01/2020
Dar es Salaam
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi amewataka wafanyakazi wa Baraza la Kiswahili Taifa kuwa wabunifu wa miradi
itakayoliletea taifa matokeo chanya katika kutangaza lugha ya Kiswahili kwenye nyanja za Kimataifa.
Dkt.Possi ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam alipotembelea ofisi za baraza hilo kwa lengo kupata taarifa za utekelezaji wa mpango mkakati wake pamoja na
kufahamu malengo ya taasisi hiyo katika kipindi cha kwanza kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
“Nawapongeza kwa mradi huu mzuri wa Kongoo sababu kazi mnayofanya yakuingiza maneno tabribani billion moja ya Kiswahili katika mtandao itasaidia sana kukuza na
kusambaza lugha hii kwani sasa dunia imejikita zaidi katika tehama na shughuli nyingi zinafanyika kwa njia ya mtandao hivyo uhifadhi wa maneno hayo ya Kiswahili katika mfumo huu ni hatua nzuri,”Dkt.Possi.
Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Kaimu Katibu Mkuu huyo aliendelea kusisitiza kuwa BAKITA ni taasisi muhimu kwa taifa na wizara ipo tayari kwa kuwawezesha kufanikiwa kutekeleza majukumu yake ya kuweza kufanikisha lugha hiyo inasonga mbele sababu kukua kwa lugha hiyo ni ufahari kwa Tanzania na haswa
kama waasisi wa kutumia hugha hiyo.
Pamoja na hayo nae Katibu Mtendaji wa BAKITA Dkt.Selemani Sewangi alitoa maombi Kaimu Katibu Mkuu huyo ya kuomba wizara iwasaidie katika kutangaza katika wizara mbalimbali kuwa wanauza Kamusi Kuu ya lugha ya Kiswahili iliyoandaliwa na baraza hilo yenye maneno mengi kwani uandaaji wa kamusi za Kiswahili ni moja ya
majukumu yao.
“Tungependa baraza lianze kutoa mafunzo ya ukalimani kwa wahitimu wa chuo kikuu na wadau mbalimbali sababu tumeona kuna ombwe kubwa la wataalamu wa lugha
wanaoweza kufanya kazi ya ukalimani hivyo tungeomba kupatiwa fedha ili kuweza kufanikisha kununua vifaa vya kutoa mafunzo hayo,”alisema Dkt.Sewangi.
Halikadhalika Dkt.Sewangi aliwashukuru uongozi wa wizara kwa kuwapa ahadi ya kushughulikia suala ya baraza hilo kupata kiwanja cha kujenga ofisi ndani ya Jiji la Dodoma ambapo ndiyo Makao Makuu ya Ofisi za Serikali.
Mbali na hayo nae mmoja wa wafakakazi wa baraza hilo ambaye ni Mfasiri Mkuu Bibi. Vidah Mutasa alitoa neno la shukrani baada kumalizika kwa kikao hicho cha kiongozi
huyo wa wizara na wafanyakazi wa baraza kwa kuahidi kuchapa kazi na kuhakikisha wao kama mabalozi wa lugha hiyo wanahakikisha inasonga mbele.