Aliyekuwa Katibu mwenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Bahi Yuda Mbata,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM,kulia kwa kwake ni Mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM wilaya ya Bahi Bw.Hassan Kadoke
Aliyekuwa Katibu mwenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Bahi Yuda Mbata,akikabidhi T-shirt yake ya chama hicho kwa Mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM wilaya ya Bahi Bw.Hassan Kadoke mara baada ya kujiunga na CCM
……………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Katibu mwenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Bahi Yuda Mbata, ameachia ngazi na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM.
Mbata ametangaza kujiondoa katika chama hicho leo jijini Dodoma huku akitaja mambo manne yaliyomfanya aondoke Chadema na kujiunga na CCM.
Ameyataja mambo hayo ni kutelekezwa na chama alipokamatwa kuhusu kuandaa maandamano ya Mange Kimambi yaliyokuwa yafanyike April 26,2018 (hata hivyo hayakufanyika).
Jambo la pili anataja kuwa Chadema kilimtelekeza katika jimbo la Chilonwa wilayani Chamwino alikokwenda kuweka misingi ya chama.
“Lakini mengine kudharirishwa na Mange akiniita ni Kibaka wa serikali na juhudi kubwa zilizofanywa na Rais Dk John Magufuli katika kuwatumikia wananchi nimeona bora kumfuata katika chama chake,” amesema Mbata.
Kiingozi huyo amesema mara nyingi chama kimekuwa kikiwashawishi kumuunga mkono Mange lakini walipoona nguvu ya mwanadada huyo imepungua wanatafuta njia ningine.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM wilaya ya Bahi Bw.Hassan Kadoke,amesema kuwa amempongeza Bw.Yuda Mbata kwa kuamua kurudi nyumbani maana nyumbani kumenoga na tunamkaribisha katika kujenga nchini inayoongozwa na Rais Magufuli kwa kauli ya hapa kazi tu.
”Kijana wenzetu ambaye alikuwa kwenye kamati za harusi mimi siwezi kuita vyama vya upinzani maana ukikaribia uchaguzi ndo unaona vinaanza kukaa hivyo navifananisha na kamati za harusi ameamua kubwaga manyanga na kuamua kurudi sisi Uvccm tunamkaribisha”amesema Kadoke
Aidha amesema kuwa wanamkaribisha kundini na watashirikiana naye na taratibu za zingine za kumkabidhi kadi zitafuata hivyo kwa sasa tuendelee kumuuga mkono Rais wetu Dkt.John Magufuli.
”Tunapenda kumwambia tu Rais wetu Dkt.John Magufuli kwa kasi yake ya kuijenga Tanzania kuwa ya Uchumi na kuendelea kuleta maendeleo kwa jamii imesababisha upinzani wilaya ya Bahi kuhamia CCM mpaka sasa hakuna upinzani tena”amesema Kadoke