Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. William Lukuvi,akizungumza wakati akifungua kikao cha dharura cha Baraza la Vyama vya Siasa kinachofanyika jijini Dodoma.

Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. Jaji Francis Mutungi,akizungumza wakati akifungua kikao cha dharura cha Baraza la Vyama vya Siasa kinachofanyika jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Ndg. Juma Ali Khatibu,akizungumza wakati akifungua kikao cha dharura cha Baraza la Vyama vya Siasa kinachofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika akichagia mada wakati wa kikao cha dharura cha Baraza la Vyama vya Siasa kinachofanyika jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. William Lukuvi,akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika wakati wa kikao cha dharura cha Baraza la Vyama vya Siasa kinachofanyika jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. William Lukuvi ametoa rai kwa Vyama vya Siasa kumtumia yeye kama daraja la kufikisha serikalini mawazo au maoni yatakayo chochea maendeleo.
Kauli hiyo ya Waziri Lukuvi ameitoa wakati akifungua kikao cha dharura cha Baraza la Vyama vya Siasa kinachofanyika mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake Juma Khatibu. Kikao hicho cha dharura kimeitishwa ili kujadili hali ya siasa nchini kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024.
Waziri Lukuvi amesema kuwa, uzoefu wake bungeni chini ya mfumo wa vyama vingi na ushiriki wake kwenye masuala mbalimbali tokea mwaka 1995 unamfanya kuwa mmoja wao na ametoa rai kwa viongozi wa vyama hivyo vya siasa kudumisha amani, maelewano na maendeleo kwa sababu vyama hivyo ni moja ya nyenzo ya kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
“Mkiwa na mambo yenu ambayo mnaona mnaweza kushiriki niambieni tu, mimi ni waziri wa siasa hivyo mkiwa na shughuli zenu huko kwenye majimbo mkinialika nakuja, nataka tujenge umoja na tuelewane” amesisitiza waziri Lukuvi.
Waziri Lukuvi amesema nia yake ni kufungua milango ya ushirikiano kwa kuvifanya vyama vya siasa kuwa karibu na serikali sio tu kwenye masuala ya siasa hata yale ya maendeleo.
Ameongeza kuwa, serikali inaongozwa na Chama Cha Mapinduzi lakini inayo wajibu wa kushirikiana na vyama vingine vya siasa kwa sababu serikali imewekwa na watu wenye itikadi zinazotofautiana.
Kuhusu utayari wa serikali kupokea masuala yatakayojadiliwa kwenye kikao hicho, Waziri Lukuvi amelihakikishia baraza hilo kuwa serikali imejiandaa kuyapokea mapendekezo yote na kuyapatia utatuzi mapema iwezekanavyo.
Mhe Lukuvi amevitaka vyama vya siasa nchini kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa serikali za mitaa na kujitokeza kupiga kura na kuchagua viongozi watakao Tatua changamoto mbalimbali kwenye maeneo yao.
“Ni muhimu kwa vyama vya siasa na anaamini vyama vyote 19 vitashiriki na kuhakikisha uchaguzi unakuwa mzuri.
“Rai yangu kwa viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wengine wa dini, mila tushirikiane kukumbusha watu wetu waende kujiandikisha hii ni haki ya kila mmoja bila kujali, chama au dini, kila mmoja ana haki ya kujiandisha na kwenda kushiriki uchaguzi, ,”amesema
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa NCCR MAGEUZI Joseph Selasini bhui amesema Mkutano huo wa dharura ni wa kwanza kufanyika katika kipindi ambacho wanajipanga kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa.
“tunampongeza Msajili wa Vyama vya siasa kwa ubunifu huu wa kuwakutanisha viongozi wa vyama vya siasa na kujadili agenda moja tu ya hali ya Siasa nchini kabla ya uchaguzi ila kusaidiana katika kuwahamasisha wananchi kujiandikisha na kujitokeza katika uchaguzi, jambo hili hata Dunia itaona nia njema ya kutaka kuona uchaguzi unakuwa huru na haki, “ameeleza Selasini



