Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe akitoa maelezo ya jumla kwa watumishi wa kituo hicho,wawakilishi wa wafanyabiashara na Viongozi wa Wilaya ya Rombo alioongozana nao katika ziara ya kutembelea kituo Cha forodha cha Holili kilichopo wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro.
…
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe amewaomba wafanyabiashara katika mipaka nchini kurasimisha Biashara yao ili watambulike katika mifumo ya kibiashara.
Mhe.Kigahe ameyasema hayo wakati akizingumza na wafanayakazi wa kituo Cha forodha cha Holili kilichopo Wilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjaro.
“Kazi ya Wizara ya Viwanda na Biashara ni kuwasaidia mazingira ya Uwekezaji na wafanyabiashara ili wafanyabiasha wawe wengi mapato yaongezeke” Amesema Kigahe
Mhe Kigahe amewaasa wafanyabiashara kurasimisha Biashara zao ili watambulike katika mifumo ya Serikali ili wafanye Biashara yao kwa uhakika mwisho wa siku Serikali ipate sehemu ya mapato yake hata kama ni kidogo kidogo.
Kigahe ,Amesema kuwa lengo la serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha wafanyabiashara wanatambulika katika mifumo rasmi ya kufanya Biashara utakaosaidia kutosumbulia pia waweze kuchangia pato la Taifa kwa kulipa kodi kama Sheria zinavyotaka.
Aidha Mhe . Kigahe ametanabaisha kuwa Serikali inafanya mpango wa kuongeza mipaka mingine rasmi ili kupunguza Biashara ya magendo inayofanyika hivi sasa inayochangia kuingiza Biashara zisizo na viwango na na zisizolipia Kodi.
Nae Afisa Mfawidhi wa kituo Cha Forodha wa kituo Cha Holili Bw.Mohamed Fukwa katika taarafia yake ya utendaji kwa Mhe Naibu Waziri amesema kuwa kituo hicho kinawafanyakazi 100 ambao wanatoka katika taasisi 12 tofauti.
Amabainisha kwamba katika kipindi cha miezi miwili (Julai 2024 hadi Agosti 2024) kituo kimeweza kukusanya jumla ya TZS. Bilioni 25.5 kati ya lengo la kukusanya ya TZS. 21.9 Hii ikiwa sawa na ufanisi wa asilimia 116.00.
Aidha ameeleza Bidhaa zinazopita mara kwa mara kutoka bandari ya Mombasa kuelekea nchi jirani kupitia mpaka wa Holili ni kuwa ni Nguo (clothes) Mafuta Ghafi (Crude Palm Oil), Sukari (Brown Sugar), Viatu (shoes), Bidhaa Mchanganyiko (Assorted items), Chupa tupu (Empty Bottle), Vipuri (Auto spare parts), Mafuta ya msingi (Base Oil),
Ethyl Alcohol, Pvc Resin na nk
Kwa upande wake mwakilishi wa wafanyabiashara wa Bw. Zuberi Shangwe amemwelezea Mhe Naibu Waziri kuwa wanakabiliwa na changamoto ya soko katika mpaka eneo la mpaka huo kwa kuwa soko lilipo kwa sasa ni dogo sana ambalo baadhi ya miundombinu yake imechakaa hivyo kuomba kijengawa soko jipya .
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe akisalimiana na watumishi wa kituo Cha Forodha Cha Holili kilichopo Wilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjaro baada ya kufanya ziara katika kituo hicho kwa lengo la kukagua shuu za Biashara zinazofanyika katika mpaka huo.
Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mhe.Reimond Mwangala
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe (Mb) akiuliza maswali watumishi wa TRA namna ya utendaji kazi katika kituo Cha forodha cha Holili kilichopo Wilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjaro
Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mhe.Reimond Mwangala na Afisa Mfawidhi wa kituo Cha Forodha Cha Holili Bw.Mohamed Fukwa mwenye koti.
Afisa Mfawidhi wa kituo Cha Forodha Cha Holili Bw.Mohamed Fukwa (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Exaud Kigahe Katikati na Mhe, Reimond Mwangala kushoto kuhusu Idara mbalimbali za Taasisi zinazofanya kazi katika kituo hicho kilichopo Wilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjaro
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara amefanya ziara ya kuangalia shughuli za kibiashara zinazofanyika katika kituo hicho na vituo vya Mpakani vyote vilivyoko Mikoa ya Kaskazini.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe akitoa maelezo ya jumla kwa watumishi wa kituo hicho,wawakilishi wa wafanyabiashara na Viongozi wa Wilaya ya Rombo alioongozana nao katika ziara ya kutembelea kituo Cha forodha cha Holili kilichopo wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro.