Kamishna wa Maadili,kutoka Sekretarieti ya maadili wa viongozi wa Umma Jaji Mstaafu,Harold Nsekela, akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma (hawapo pichani)wakati akitoa tathmini ya hali ya urejeshaji wa tamko la rasilimali na madeni ya viongozi wa umma.
Kamishna wa Maadili,kutoka Sekretarieti ya maadili wa viongozi wa Umma Jaji Mstaafu,Harold Nsekela, akionyesha karatasi kwa Waandishi wa Habari jijini Dodoma (hawapo pichani)wakati akitoa tathmini ya hali ya urejeshaji wa tamko la rasilimali na madeni ya viongozi wa umma.
Kamishna wa Maadili,kutoka Sekretarieti ya maadili wa viongozi wa Umma Jaji Mstaafu,Harold Nsekela,akisisitiza jambo kwa Waandishi wa Habari jijini Dodoma (hawapo pichani)wakati akitoa tathmini ya hali ya urejeshaji wa tamko la rasilimali na madeni ya viongozi wa umma.
Mwaandishi wa habari kutoka gazeti La Jiji Bw.Moses Ngw’ati akiuliza swali kwa Kamishna wa Maadili,kutoka Sekretarieti ya maadili wa viongozi wa Umma Jaji Mstaafu,Harold Nsekela,alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari jijini Dodoma wakati akitoa tathmini ya hali ya urejeshaji wa tamko la rasilimali na madeni ya viongozi wa umma.
Kamishna wa Maadili,kutoka Sekretarieti ya maadili wa viongozi wa Umma Jaji Mstaafu,Harold Nsekela, akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari jijini Dodoma (hawapo pichani)wakati akitoa tathmini ya hali ya urejeshaji wa tamko la rasilimali na madeni ya viongozi wa umma.kulia ni Katibu Idara ya Usimamizi wa Maadili John Kaole
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
…………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Kamishna wa Maadili,kutoka Sekretarieti ya maadili wa viongozi wa Umma Jaji Mstaafu,Harold Nsekela ,amesema kuwa jumla ya viongozi wa umma 11,330 sawa na asilimia 83 hadi kufikia Desemba 20 mwaka huu bado hawajarejesha tamko la rasilimali na madeni ya viongozi wa umma kwa Kamishna wa Maadili.
Hayo ameyasema leo jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akitoa tathmini ya hali ya urejeshaji wa tamko la rasilimali na madeni ya viongozi wa umma.
Kamishna Nsekela amesema kuwa hadi kufikia Desemba 20 mwaka huu, tathmini inaonesha kwamba hali ya urejeshaji mpaka sasa sio nzuri.
Nsekela amesema sheria ya maadili ya viongozi wa umma namba 13 ya mwaka 1995 fungu la 9 (1) (a)-(c) linamtaka kila kiongozi wa umma aliyetajwa katika fungu la (4) kuhakikisha anawasilisha madeni na rasimali zake katika hati rasmi.
Amesema sheria hiyo inamtaka kila kiongozi wa umma aliyetajwa kuorodhesha kwa kamishna wa maadili rasimali zake au Mume au watoto wenye umri usiozidi miaka 18 na ambao hawajaoa au kuolewa ikiwa ni kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (2) na kile kingine cha (5).
” Kiukweli viongozi ambao wameshawasilisha matamko yao ni wachache sana jambo ambalo halileti taswira nzuri kwa sababu Nchi yetu imekua ikisisitiza suala la utawala bora na kufuata sheria.
Tumetumia muda mrefu kukumbushana na hata mimi mwenyewe katika siku ya maadili nilizungumzia umuhimu wa viongozi kuwasilisha matamko yao lakini mpaka sasa hali siyo nzuri,” Amesema Jaji Mstaafu Nsekela.
Jaji Mstaafu Nsekela amesema ni wazi tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Magufuli kumekuwepo na usimamizi mzuri wa rasimali za Nchi hivyo kitendo cha viongozi wa umma kushindwa kuwasilisha taarifa zao ni kurudisha nyuma maendeleo na jitihada zinazofanywa na Mhe Rais.
Amesema kushindwa kuwasilisha tamko la rasimali na madeni katika muda uliowekwa kisheria ni kosa chini ya fungu la 15 (a) hivyo kiongozi yeyote ambaye hatowasilisha tamko lake Sekratarieti ya Maadili haitosita kuchukua hatua za kisheria ikiwemo kumfikisha katika baraza la maadili.
” Naomba ieleweke pia Sheria ya maadili inakataza kiongozi ambaye atawasilisha taarifa za uongo kwani akifanya hivyo atakua ametenda kosa na akitiwa hatiani atatozwa faini ya Sh Milioni Moja na si zaidi ya Sh Milioni Tano au kifungu kisichozidi mwaka mmoja,” Amesisitiza
Aidha, amesema kuwa mwaka kesho wataanza kutumia njia ya mtandao kupokea matamko.
“Mwaka kesho wote tunaingia katika mtandao na mambo yote yamekaa vizuri kuna leseni ambayo tunatakiwa kuwa nayo na tutaipata.Mwaka kesho hatuingii kwenye matamko kama haya kitakuwa kila kitu kimeisha,”amesema Jaji Mstaafu Nsekela