Waziri wa Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo akizindua wiki ya AZAKI Mkoani Arusha

Happy Lazaro, Arusha
Waziri wa Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amesema serikali haitakuwa kikwazo kwa shughuli zinazoendeshwa na asasi za kiraia (AZAKI) na kuwataka kuwa na jukumu la kutafuta fursa zaidi katika kujipatia maendeleo.
Akizindua maadhimisho ya AZAKI yaliyokutanisha washiriki zaidi ya 600 yanayofanyika jijini Arusha ,Prof Mkumbo amesema lengo la Dira ya Taifa kwa miaka 25 ijayo ni kuondoa umaskini na kuweka ustawi kwa wananchi wote kwa serikali kuanza kuwekeza katika elimu zaidi.
Prof .Mkumbo amesema kuwa,serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa asasi hizo na kamwe haitakuwa kikwazo kwa shughuli za Asasi za kiraia zinazoendelea hapa nchini .
Amesema asasi za kiraia zina jukumu la kutafuta fursa kwa serikali ,sekta binafsi pamoja na Asasi, hivyo serikali itakuwa pamoja nao na kuwaunga mkoani .
Naye Rais wa Shirika la Foundation for Civil Society FCS Dkt. Stigmata Tenga amesema asasi ni daraja kati ya sauti za mwananchi ,dira za wananchi na thamani ya mwananchi hivyo kwa muda wa wiki moja watakaa pamoja wataongelea namna watakavyofanya kazi ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Ameongeza kuwa rasili Mali watu ndo nguvu kazi na ndio inayoweza kuleta mabadiliko na kuhakikisha mwananchi wa Tanzania ameweza kuendesha maendeleo yake mwenyewe bila kusaidiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Foundation for Civil Society ,Justice Rutenge amesema kuwa , wanahitaji kufanya kazi kwa pamoja ili kuondoa vikwazo vilivyopo na kushughulikia changamoto za kimuundo na kimfumo na kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.
“Tunataka kuvuka vikwazo vikubwa kwa kufanya kazi pamoja ili kuondoa vikwazo kama afya, kilimo, biashara na utawala bora kwani Sisi kama wadau tuna maoni mengi sana ya kuweza kuchangia ili kuendana na kasi ya dira ya maendeleo. “
