Dar es Salaam
Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Balozi, Mhandisi, Aisha Amour ameupongeza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kusaidia program ya Wahandisi wataraji (Structured Engineers Apprenticeship programe) wapatao 428 kote nchini ili kupata mafunzo ya kuwajengezea uwezo kukuza tasnia yao.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya 21 ya siku ya Wahandisi nchini yanayofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es salaam Balozi Amour alisema TARURA inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wahandisi wataraji wapatao 428 wakifuatiwa na TANROADS (251),TTCL(164), RUWASA (156) na TANESCO (126).
“Naipongeza sana TARURA ni Taasisi inayoongoza kwa kuwapokea wanafunzi wengi wanokuwa katika program hii, tatafurahi na Taasisi nyingine nazo kujitokeza”, amesisitiza Katibu Mkuu