Bi.Alestidia Ngalaba kutoka ofisi ya Mdhibiti na Mkuguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali akisoma hotuba katika Warsha ya Wahariri wa Vyombo vya habari na namna ya kuripoti taarifa za CAG.
Mchumi kutoka Ofisi za CAG Bw.Emmanuel Philipo akiwasilisha Mada katika Warsha ya Wahariri wa Vyombo vya habari na namna ya kuripoti taarifa za CAG.
Wanahabari wakifuatilia Mada zinazowasilishwa katika Warsha ya Wahariri wa Vyombo vya habari na namna ya kuripoti taarifa za CAG.
********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Wanahabari wametakiwa kuandika na kuripoti taarifa za ofisi za CAG kwa ufasaha ili kuweza kuwaelimisha wadau na wananchi kwa ujumla namna ya kusimamia raslimali na fedha kwa ajili ya maendeleo.
Akizungumza katika Semina ya Wanahabari juu ya kuandika taarifa za Ofisi za CAG katika vyombo vya habari Bi.Alestidia Ngalaba amewataka wanahabari kupitia vyombo vyao kusaidia kuchambua kwa ufasaha kwa kutumia lugha nyepesi ambayo kila mwananchi ataweza kuielewa vizuri na kufanya maamuzi sahihi ya kusimamia matumizi mazuri ya raslimali za taifa.
“Sambamba na warsha hii kwa miaka iliyopita mafanikio tuliyapata ni pamoja na kuweza kufanya kazi kwa pamoja na vyombo vya habari kwa ukaribu zaidi.Hii imesaidia kuboresha kazi za kikaguzi ambazo zinasaidia kuleta maendeleo ya nchi kwasababu kila mmoja anajifunza jinsi ya kutumia na kulinda raslimali zetu ambazo zinatokana na kodi zetu sisi wenyewe”. Amesema Bi.Alestidia.
Nae Mwakilishi wa Msemaji Mkuu wa Serikali Bw.Elias Malima amewataka Wanahabari kutumia mitandao ya kijamii vizuri katika uandaaji wa habari na wasitegemee kupata taarifa kupitia mitandao ya kijamii kwani taarifa nyingi katika mitandao ya kijamii hupotosha jamii.
Kwa upande wake Mchumi kutoka ofisi ya CAG, Bw.Emmanuel Philipo akiwasilisha mada isemayo Ijue Ofisi ya Taifa Ukaguzi amewataka wanahabari kufahamu namna ya kuandika taarifa za ofisi ya CAG ili kuweza kuwapa wananchi fursa ya kutoa maoni yao kuhusiana na utendaji kazi wa ofisi ya taifa ya Ukaguzi.
“Lengo la warsha hii ni kusambaza na kupata mrejesho wa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali toleo la wananchi napia kuwaamasisha wadau kushirikiana na mkaguzi mkuu wa Nje (CEA) katika maeneo yao ikudumisha ukguzi shirikishi”.Amesema Bw.Philipo.