Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua skimu ya Umwagiliaji ya Makwale iliyopo katika kata ya Makwale Wilayani Kyela, leo tarehe 20 Disemba 2019 wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Mbeya. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua skimu ya Umwagiliaji ya Makwale iliyopo katika kata ya Makwale Wilayani Kyela, leo tarehe 20 Disemba 2019 wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Mbeya.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akishuhudia mnada wa Kakao katika kijiji na kata ya Ikolo ambapo Kakao imeuzwa kwa bei ya shilingi 5042 kwa kilo moja, leo tarehe 20 Disemba 2019 wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Mbeya.
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Kyela
Kilimo-Kyela
Waziri wa
Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 20 Disemba 2019 amepiga marufuku
madalali wa mazao ya kilimo ambao wanatumia nafasi hiyo kuwagalaliza wakulima.

Waziri
Hasunga amepiga marufuku hiyo wakati akizungumza kwenye mnada wa Kakao
uliofanyika kwenye kijiji na kata ya Ikolo iliyopo katika Wilaya ya Kyela
wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Mbeya.

Amesema
kuwa “kumekuwa na wananchi wasiokuwa waaminifu kwa serikali na wakulima
wake ambao wanawaibia wakulima maarufu kama Njemke, Butura, na Kangomba hivyo
napiga marufuku biashara hiyo na endapo tukiwakamata tutawachukulia hatua za
kisheria”

Hasunga amewaagiza wanunuzi hao wa Kakao na mazao mengine kuhakikisha kuwa
wanawalipa wakulima fedha zao mara baada ya kukamilika kwa minada ili waweze
kupata fursa ya kuandaa mashamba katika kipindi hiki cha msimu wa kilimo.

Hasunga amesema kuwa zao hilo la Kakao litasalia kuuzwa kupitia mfumo wa
stakabadhi ghalani kwani kupitia mfumo huo ambao unasimamiwa chini ya Tume ya
Maendeleo ya Ushirika wakulima wataendelea kunufaika na mazao yao kwa kupata
bei nzuri.

kuwa bado vyama vya ushirika vina matatizo makubwa lakini serikali itaendelea
kusimamia kwa weledi vyama hivyo ikiwemo kuchukua hatua za haraka kwa viongozi
wa vyama hivyo wanaotumia vibaya nafasi yao kwa kuwaibia wakulima.

Amevitaka
Vyama vikuu vya ushirika wa Kakao kuwa pamoja na kusimamia ubora wa zao hilo lakini
pia amesema kuwa vyama hivyo vinapaswa kuendelea kuhamasisha wadau mbalimbali
kuanzisha viwanda vya kuchakata Kakao ikiwa ni sehemu muhimu ya kuunga mkono
juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe
Magufuli kwa kuhamasisha sekta ya viwanda.

Amesema kuwa Kakao inayolimwa wilayani kyela nchini Tanzania ni
miongoni mwa Kakao bora Duniani ambayo ina ubora mzuri kuliko Kakao nyinyine
zinazozalishwa katika nchi za Afrika Magharibi.

Waziri Hasunga ameshuhudia mnada wa Kakao katika kijiji na kata ya Ikolo ambapo
imeuzwa kwa bei ya shilingi 5042 kwa kilo moja ambapo
amesisitiza kuwa bei hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa wakulima.

Sambamba na hayo Mhe Hasunga amewasihi wakulima kuendelea
kulima zao hilo huku akiahidi kuwa serikali kupitia wizara ya kilimo itaendelea
kusimamia kwa weledi kuongeza tija na uzalishaji.