Viongozi na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi wameishukuru sana Serikali kwa kuwapatia fedha za miradi ya barabara za mjini, dampo, gari la kuzoa taka, pamoja na ujenzi wa machinjio ya Kisasa. Shukran hizo zimetolewa leo wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo mkoani Lindi.
Halmashauri ya Manispaa ya Lindi ni miongoni mwa halmashauri 18 zinazo tekeleza mradi wa ULGSP hapa nchini ambapo kwa Manispaa ya Lindi imewezeshwa Dola za Kimalekani Milion tano kutekeleza miradi yake.
Katika ziara hiyo Waziri Jafo alifanya ukaguzi wa machinjio ya Kisasa na amepongeza sana kazi nzuri iliyofanywa na Manispaa hiyo katika utekelezaji wa miradi yake