***********************************
NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO
SERIKALI wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, imeanzisha vita dhidi ya dawa za kulevya kwa vijana, ikiwa na lengo la kuwanusuru vijana waondokane na athari ya matumizi ya madawa hayo..
Akizundua mpango huo, mkuu wa wilaya hiyo Zaynabu Kawawa alisema, kwenye fukwe za Bahari ya Hindi zilizoko mjini hapo aliwaasa, walengwa kuachana na dawa za kulevya kwani zina madhara ya kiafya na kuwaondolea utu wao.
“Vijana wenzangu niwaombe muachane na matumizi ya dawa za kulevya, kutokana na kujiingiza katika matumizi hayo mmekuwa mkitengwa na jamii kutokana na kujiingiza kwenye matumizi hayo,” alisema Zaynab.
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Mradi huo Dr. Eric Aris aliishukuru ofisi ya Mkuu huyo kwa kuukubali mpango huo, unaoratibiwa na Serikali ya watu wa Marekani.
Alisema kwamba wamejionea vijana waliobadilika kwa kuachana na matumizi ya dawa.
“Tulifika katika ofisi yako tukazungumzia kuhisiana na zoezi hili, tunakushukuru binafsi ukishirikiana na wataalamu wako mmeukubali mpango huu, na leo tuko hapa na vijana walioachana na matumizi ya dawa za kulevya tumewaona,” alisema Dr. Aris.
Mratibu wa dawa za kulevya wilayani Bagamoyo Husna Kipilipili ,alisema kikundi cha Umoja wa Vijana Walioacha Dawa za Kulevya Bagamoyo (UVIWAMABA) kimechaguliwa Kitaifa kuwa kikindi kitachowabaini vijana wanaitumia dawa hizo wilayani hapa.
“Mpango wetu wa kuwapatia huduma za dawa za Mesadol zitaanza rasmi wilayani Bagamoyo Desemba 16 kuanzia hatua hii itawapatia nafasi walengwa kuwa na muda wa kwenda kuendelea na shughuli zao za kujipatia kipato.