Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Kiwanda cha kuunganisha Matrekta katika eneo la Nzuguni wakati wa Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane, tarehe 08 Agosti, 2024.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la Msingi ujenzi wa Viwanja vya Maonesho ya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma tarehe 08 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiangalia bidhaa mbalimbali za kilimo zilizotokana na bustani zilizopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma tarehe 08 Agosti, 2024. Bustani hizo zimetumia mbolea za ndani na nje ya nchi ili kuwaonesha Wakulima tija ya mbolea za ndani.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mfano wa Ufunguo Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe kama ishara ya makabidhiano ya Zana za mbalimbali za Kilimo Matrekta 519, Power Tiller 800, Majembe ya kulimia 200 wakati wa kilele cha Maonesho ya Wakulima Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma tarehe 08 Agosti, 2024.
 Matukio mbalimbali katika picha za hafla ya Kilele cha Maadhimisho ya Sikuu Kuu ya Wakulima ( Nanenane) ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alitembelea mabanda mbali mbali na kulihutubia Taifa katika viwanja vya Maonesho hayo, Nzuguni Jijini Dodoma tarehe 08 Agosti, 2024.