Viongozi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL wametembelea wateja waliounganisha na huduma ya Faiba katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni-Dodoma.
Lengo ni kupata mrejesho juu ya huduma hiyo na kuwashukuru kwa kutumia huduma hiyo wakati wa maonesho
Naye Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima (NHIF) Dodoma Bw.Fidelis Shauritanga amesema wanafurahia huduma ya Faiba waliyofungiwa na imewasaidia sana katika kufanikisha majukumu yao wakiwa katika Viwanja hivyo.
“Huduma hii ni nzuri sana imetusaidia tunafanya kazi kama tupo ofisini na hata nyumbani kwangu ipo na naitumia pamoja na familia yangu.”Amesema Fidelis

