Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Nelson Mlali wakiwa katika ziara ya kukagua na kusikiliza changamoto za Bandari kavu ya Hami Logistics pamoja na Bravo Logistics iliyofanyika Agosti 7, 2024, jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile akizungumza na waandishi wa habari wakati akiwa katika ziara ya kukagua na kusikiliza changamoto za Bandari kavu ya Hami Logistics pamoja na Bravo Logistics iliyofanyika Agosti 7, 2024, jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Nelson Mlali akizungumza na waandishi wa habari wakati akiwa katika ziara ya kukagua na kusikiliza changamoto za Bandari kavu ya Hami Logistics pamoja na Bravo Logistics iliyofanyika Agosti 7, 2024, jijini Dar es Salaam.

Picha za matukio mbalimbali wakati Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Nelson Mlali wakiwa katika ziara ya kukagua na kusikiliza changamoto za Bandari kavu ya Hami Logistics pamoja na Bravo Logistics iliyofanyika Agosti 7, 2024, jijini Dar es Salaam.
………………
Serikali imesema ipo katika mipango ya kuboresha mifumo ya utoaji huduma sekta binafsi ikiwemo kutengeneza mazingira rafiki katika nyanja mbalimbali jambo ambalo lisaidia kuongeza tija kwa kuongeza mapato kupitia kodi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Agosti 7, 2024 akiwa katika ziara ya kukagua na kusikiliza changamoto za Bandari Kavu ya Hami Logistics pamoja na Bravo Logistics, Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile, ameipongeza jitihada zinazofanywa na kampuni hizo ikiwemo kuunga mkono juhudi za serikali katika kujenga uchumi wa Taifa.
Mhe. Kihenzile amesema kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo Bandari, Meli, Reli pamoja na Viwanja vya ndege.
“Wanafanya kazi kubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo kulipa kodi ambayo inatumika kujenga miundombinu ya barabara, kutoa huduma ya maji, umeme pamoja na kupunguza msongamano wa mizigo bandarini” amesema Mhe. Kihenzile.
Mhe. Kihenzile amesema kuwa wanakwenda kulifanyia kazi ombi la sekta binafsi kuhusu madai yao ya kutaka serikali kufikilia namna ya kuongeza muda wa leseni zao kutoka mwaka mmoja hadi miaka mitano kutokana wanashindwa kuandaa vizuri mipango yao ya biashara ya muda mrefu kwa ajili kuomba mkopo katika taasisi za fedha.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Nelson Mlali, amesema kuwa usafirishaji kwa njia ya maji kuna wadau wengi ikiwemo bandari kavu, hivyo wamekuja kuona utendaji kazi wao baada ya kupewa majukumu na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).
“Tumekuja kuona wamejipangeje kutoa mchango wa kuendeleza uchumi wa Taifa, tumeona mambo mengi mazuri wanayofanya, pia tumesikiliza changamoto zao na zinakwenda kutatuliwa” Bw. Mlali.
Amesema kuwa TASAC wana jukumu la kuwapa leseni wanaofanya biashara hizo na wamekuwa na utamaduni wa kuwatembelea mara kwa mara kwa ajili ya kuwakagua ili kuona wanatekeleza masharti ya leseni zao.
Nao Hami Logistics pamoja na Bravo Logistics wamefurahia ujio wa Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile ambapo wamepata fursa ya kueleza changamoto zao katika kuhakikisha wanaendelea kufanya kazi kwa ufanisi na kuchangia katika pato la Taifa.
