WANANCHI mbalimbali wakipata elimu Wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA) walipotembelea banda la BRELA wakati Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
………….
Na.Alex Sonna-DODOMA
WANANCHI wa Mkoa wa Dodoma pamoja na viunga vyake wametakiwa kutembelea katika viwanja vya maonesho ya kilimo nanenane hususani katika banda la Wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA) kwa ajili kupata uelewa juu ya umuhimu wa kusajili bidhaa zao.
Ameeleza kuwa wananchi wanaweza kutatuliwa changamoto zao pamoja kupatiwa elimu sahihi pale ambapo watafika katika banda hilo kwa lengo la kujengewa uwezo na kupata huduma ya usajili wa bidhaa zao na kwa kuziongezea ubora bidhaa hizo.
Akizumgumza na wananchi na waandishi wa habari Afisa Kumbumbukumbu BRELA,Farid hoza amesema mwananchi akifika katika banda hilo watapata uelewa zaidi juu ya umuhimu wa kusajili bidhaa ambazo wanazizalisha na kuziongezea ubora kwa kiwango kinachokubalika.
“Tunawasaidia wanawasaidia wakulima, wafanyabishara kuweza kufanya maombi yao ya usajili.
” Katika haya maonesho tunafanya usajili wa papo kwa papo kitu ambacho sio rahisi na kama ulikuwa na changamoto ya muda mrefu haitatuliki ukija kwenye banda letu la Brela tunakusaidia Baraka, ” Amesema
Na kuongeza ” Tunatoa elimu kitu ambacho unaweza usikipate ukiwa nyumbani lakini ukija hapa tunakupa elimu, ” Amesema Afisa kumbukumbu huyo.
Pia amesema kwamba kutokana na umuhimu wa kujisajili wamekuwa wakitembea mikoani mbalimbali kutoa elimu ambapo mpaka sasa wanufaika niwengi kwani wameshatembea takribani mikoa yote ya Tanzania pamoja na kuwafikia wakulima na wafanyabishara na bado wanaendelea kwani zoezi hilo ni endelevu.
Mpaka sasa waneshasajili makampuni zaidi ya 50 kwenye maonesho hayo ya nanenane.
“Wito wananchi kuudhuria katika maonesho ili kusajili biashara zao unaposajili unatambulika kisheria
Wapo kwenye maonesho ya kimatifa ya kilimo yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni ambapo wapo kutoa huduma za usajili wa majina ya biashara, usajili wa makampuni,usajili wa alama za bishara na usajili wa Ataza na usajili wa leseni kundi A