Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Mhe. George Simbachawene akijadili jambo na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kabla ya kufungua mafunzo ya namna ya kusajili wanachama wa Chama cha Mapinduzi kwa njia ya kielektroni.
Baadhi ya Watendaji wa CCM wa kata zote katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati wa mafunzo ya namna ya kusajili wanachama wa Chama cha Mapinduzi kwa njia ya kielektroni.

Na. Mwandishi Wetu
“Tunampongeza Rais na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu wa Chama Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa kuja na mpango huu wa kusajili wanachama kwa njia ya kidijitali.
Ninaamini tukijituma na tukakamilisha utekelezaji wa mpango huu kwa ufanisi, tutakuwa tumetendea haki maono ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu wetu na chama kitakuwa imara zaidi”
Pongezi hizo zilitolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Mhe. George Simbachawene tarehe 4 Agosti, 2024 wakati akifungua mafunzo ya namna ya kusajili wanachama wa Chama cha Mapinduzi kwa njia ya kielektroni katika ofisi za CCM Wilaya Mpwapwa yanayohusisha Watendaji wa CCM wa kata zote katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.
Mhe. Simbachawene aliongeza kuwa nyuso na wingi wa washiriki waliohudhuria ni imani tosha kuwa wapo tayari kupokea mafunzo na kutekeleza majukumu hilo kwa haraka na ufanisi.
“Mimi ndiye mwenye dhamana ya kusimamia TEHAMA Serikalini, ninajua utamu na urahisi wa kutumia TEHAMA katika utoaji wa huduma kwa umma. Hivyo, nimefurahi kuona pia Chama chetu Cha Mapinduzi kikisajili wanachama wake kwa njia ya kidijitali, Mwelekeo huu ni mzuri na kutakuwa na taarifa sahihi za wanachama kwa kubofya tu” aliongeza Mhe. Simbachawene.
Hali kadhalika Mhe. Simbachawene alisema kuwa tangu Dkt. Samia alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM amefanya mambo makubwa ikiwa ni pamoja na kutoa vitendea kazi kwa watendaji wote wa Chama, mathalani magari na pikipiki ili kuwafikia wanachama kwa urahisi na hivyo kuimarisha chama kwa kuzingatia misingi ya utawala bora.
Alibainisha kuwa, vitendea kazi hivyo hususani Pikipiki ambazo hata Wanampwapwa kwa ngazi zote za kata na jumuiya wamenufaika nazo ni kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchama na kutekeleza Ilani na si kuzifanya kuwa boda boda.
Aidha, ametoa rai kwa watendaji hao kusikiliza kwa makini na kufuata maelekezo ya wakufunzi ili zoezi hilo likamilike kwa ufanisi na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wanachama na kudhibiti matumizi mabaya ya uanachama kwa baadhi ya watu.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mpwapwa Bw. Dennis Luhende Mbulu amewaomba watendaji hao kuzingatia rai hiyo na amemshukuru Waziri na Mbunge Mhe. George Simbachawene kwa kufungua zoezi hilo muhimu kwa Wilaya ya Mpwapwa na kwa ustawi wa Chama Cha Mapinduzi.