Na
Mwandishi Wetu, Morogoro
UONGOZI
wa Machinjio ya Nguru Ranch Hills, umempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Sera zake nzuri za biashara na
uwekezaji, zilizopelekea ufanisi katika uendeshaji wa Machinjio hayo ya kisasa
nchini.
Shukrani
hizo zimetolewa na Meneje Mkuu wa Machinjio hayo, Bw. Eric Cormack, wakati Rais
Samia alipotembeela banda la Nguru Hills Ranch, wakati wa uzinduzi wa kampeni
ya Tutunzane, kwenye viwanja vya Sokoine Wilayani Mvomero Agosti 3, 2024.
Machinjio
ya Nghuru Hills Ranch yanamilikiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi
wa Umma (PSSSF) na wabia wengine wawili, Eclipse Investment LLC kutoka Oman na Busara
Investment LLP ya hapa nchini.
“Hizi
zote ni juhudi zako kwenye Public Private Partnership, tunakushukuru sana kwa
hilo na haya ni matunda ya wazi kabisa, juhudi zako zimesaidia kufungua masoko,
wateja wetu wamekuwa wakitueleza,” alisema Bw. Cormack.
Aidha,
Mhe. Rais Dkt. Samia, alipata fursa ya kuelezwa hatua kwa hatua za utekelezaji
wa shughuli za Machinjio, kuanzia Ufugaji (Unenepeshaji mifugo), Uchinjaji, na
Ufungashaji wa nyama kwa ajili ya usafirishaji kwenda kwenye masoko ya ndani na
nje ya nchi.
Pia
Bw. Cormack alimueleza Rais Samia kuwa Machinjio hayo yanafuata taratibu za
Halal (Australia Halal Certification) hatua iliyosaidia kuaminika kwenye masoko
ya nje hususan nchi za Ghuba (Gulf Cooperation Council-GCC), ambazo ni pamoja
na Bahrain, Kuwait, Oman, Qatar, Saudi Arabia, na The United Arab Emirates.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipata
maelezo kutoka kwa Meneja Mkuu wa machinjio ya kisasa ya Nguru Hills, Bw. Eric
Cormack juu ya uzalishaji wa bidhaa za nyama ambazo zinauzwa ndani na nje ya nchi, wakati wa uzinduzi wa
Kampeni ya Tutunzane, wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro tarehe 03 Agosti,
2024. Machinjio hayo yanaendeshwa na
PSSSF pamoja na wabia wengine.