RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Hodhi la Kuhifadhia Maji katika viwanja vya Maonesho ya Kilimo Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A”Unguja wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Kilimo ya Nanenane uliofanyika leo 3-8-2024,na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Muwakilishi wa Taasisi ya AATIF Rashid Ali Rashid, kuhusiana na Kilimo cha mbogamboga wakati akitembelea Maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Unguja, aliyoyafungua leo 3-8-2024 katika viwanja hivyo na (kulia kwa Rais) Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ,Umwagiliaji,Maliasili na Mifugo Ndg.Ali Khamis na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrissa Kitwana Mustafa.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Afisa Mifugo Muandamizi Bi. Zehra Karim Zam, akitowa maelezo ya ufugaji wa Kuku, wakati akitembelea banda la maonesho la Idara ya Maendeleo ya Mifugo Zanzibar, katika maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Unguja. aliyoyafungua leo 3-8-2024 katika viwnja hivyo.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa amemshika Kaa wakati akipata maelezo ufugaji wa Kaa kutoka kwa Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Khamis Bakar Khamis, wakati akitembelea banda la maonesho la Chuo cha Mafunzo Zanzibar, katika viwanja vya Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Unguja, wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane aliyoyafungua leo 3-8-2024 katika viwanja hivyo.(Picha na Ikulu)