Majambazi wawili wenye silaha wameuwawa na mmoja kufanikiwa kutoroka baada ya kurushiana risasi na askari usiku wa kuamkia jana wakati wakijaribu kufanya uvamizi katika kituo cha mafuta mjini Makambako mkoani Njombe.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Njombe Salum Hamduni amesema jeshi lilifanikiwa kuwadhibiti majambazi hao wanaokadiliwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 30 hadi 45 ambao walikuwa na siraha aina ya gobole iliyotengenezwa kienyeji kwa muundo short gun na risasi 11 za short gun huku pia akidaiwa kwamba jambazi mmoja amefanikiwa kutoroka na gari ndogo aina ya Special na kudai kwamba katika uchunguzi wa awali inaonyesha wametokea mkoani Iringa .
Aidha Kamanda Hamduni Amesema jeshi hilo pia limefanikiwa kuwakamata watuhimiwa 9 wa wizi wa mafuta katika mradi wa ujenzi wa barabara wa Moronga Makete ambapo zaidi ya lita 480 za disel na lita 400 za petroli zimekutwa baada ya msako na kwamba watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.
Jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata pikipiki 8 huku mtuhumiwa Charles Fute , Sadick Homange na John Mfikwa wakitajwa kuhusika huku hatua hiyo ikielezwa kuwa imesababishwa na ushirikiano mzuri baina ya jeshi na wananchi.