Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew J. Mtigumwe anawatangazia wananchi na wadau wa kilimo nchini kuhusu kufanyika kwa uzinduzi wa Mkakati wa Kuendeleza Zao la Mpunga Awamu ya Pili (National Rice Development Strategy Phase II).
Mkakati huo utatekelezwa kwa kipindi cha miaka kumi (10) kuanzia mwaka 2019/2020 hadi mwaka 2029/2030. Uzinduzi huo utafanyika tarehe
16 Desemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa St. Gaspar Jijini Dodoma kuanzia saa 2.00 asubuhi.
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo atakuwa Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Japhet Hasunga (Mb). Wadau wa zao la mpunga na wananchi mnaalikwa kuhudhuria kwenye uzinduzi huo.