Baadhi ya wafanyabiashara wa Soko la Magomeni lililoko Kata ya Kirumba Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza wamebomolewa meza zao zakufanyia biashara baada ya kuzitelekeza kwa muda mrefu.
Zoezi hilo la ubomoaji limefanyika leo Jumatano Julai 17, 2024.
Wakizungumza na Fullshangwe Blog baadhi ya wafanyabiashara waliobomolewa meza zao wamesema uamuzi huo umekuwa ni wa haraka sana kwani kunawengine wanauguliwa hivyo kushindwa kuendelea na biashara zao.
Kwaupande mwenyekiti wa Soko hilo Ramadhani Maganga ametoa wito kwa wafanyabiashara kulinda maeneo yao ya biashara hatua itakayosaidia kuepukana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya kubomolewa.
Akizungumzia zoezi hilo la ubomoaji kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaaa ya Ilemela, Afisa biashara wa Manispaa hiyo Yohannes Daud, amesema wafanyabiashara hao wamezitelekeza meza hizo huku wengine wakikosa sehemu za kufanyia biashara.