Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akipeana mkono na Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Pascal Karomba wakati wa makabidhiano ya Tuzo ya Uandaaji bora wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2018 ambapo Ofisi ya Makamu wa Rais imeshika nafasi ya tatu. Tuzo hiyo imetolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA).
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wahasibu mara baada ya kukabidhi tuzo hiyo Ofisini kwake jijini Dodoma. Tuzo hiyo imetolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA).
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akipokea tuzo ya Uandaaji bora wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2018 kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa
Ofisi hiyo Bw. Pascal Karomba ambapo Ofisi ya Makamu wa Rais imeshika nafasi ya tatu. Tuzo hiyo imetolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA).