Mwenyekiti wa Bodi Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) Profesa Ulingeta Mbamba akizungumza leo Julai 9, 2024, Dar es Salaam katika Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Misri lililofanyika katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba.
Balozi wa Misri nchini Tanzania, Bw. Shariff Ismail akizungumza leo Julai 9, 2024, Dar es Salaam katika Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Misri lililofanyika katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) Bi. Latifa Khamis akizungumza leo Julai 9, 2024, Dar es Salaam katika Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Misri lililofanyika katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba.
Meneja Uenezi na Masoko, Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Bw. Khamis Dunia akizungumza leo Julai 9, 2024, Dar es Salaam katika Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Misri lililofanyika katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba.
Afisa Biashara Mwandamizi Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) Bi. Mariam Kikoti akizungumza leo Julai 9, 2024, Dar es Salaam katika Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Misri lililofanyika katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba.
t
……….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Serikali kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) imesema itaendelea kushirikiana na Nchi ya Misri katika masuala ya biashara ili kuhakikisha wafanyabiashara wanaendelea kupata fursa za kupeleka bidhaa mbalimbali nchini humo.
Akizungumza leo Julai 9, 2024 katika Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Misri kwenye Maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa Sabasaba, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) Profesa Ulingeta Mbamba amesema kuwa Tanzania ipo kwenye nafasi nzuri ya kupeleka bidhaa za chakula, umeme na biashara zingine nchini Misri.
Profesa Mbamba amesema kuwa takwimu zinaonesha kuwa Tanzania inapekela bidhaa zenye thamani ya shillingi dola milioni moja, huku Misri zikileta bidhaa nchini Tanzania zenye thamani dola milioni 60.
“Sku ya leo imetoa fursa kwa wafanyabiashara kuonesha nini ambacho wanafanya a katika nchi hizo mbili, Tanzania invitu vingi vya kujifunza na kupeleka Misri ikiwemo masuala ya chakula, vitu vya umeme na biashara nyingine” amesema Profesa Mbamba.
Profesa Mbamba amesema kuwa mikutano ya kibiashara kati ya nchi hizo itaendelea kufanyika ambayo inaendelea kuleta tija katika biashara kati ya nchi hizo.
Balozi wa Misri nchini Tanzania, Bw. Shariff Ismail, amesema kuwa kupitia mkutano huo, matunda yataonekana baina ya nchi hizo mbili kupitia ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji katika kukuza uchumi.
Amesema kuwa ni muhimu kwa nchi ya Misri na Tanzania kwani mpaka kufikia sasa tunaadhimisha miaka 60 ya uhusiano , katika historia tunauhisiano imara.
“Kama balozi tunatafuta njia za kuimarisha uhusiano wetu kwa sababu watu wetu na historia yetu inastahili kushirikiana” amesema Bw. Ismail.
Amebainisha kuwa maonesho ya sabasaba ya mwaka 2025 anatarajia kuona idadi kubwa ya makampuni kutoka misri kushiriki nchini Tanzania.
Meneja Uenezi na Masoko, Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA),Bw. Khamis Dunia amesema kuwa mwamko ni mzuri kwa nchi ya Misri kwani kuna taasisi 36 zimeshiriki katika maonesho ya Sabasaba ya mwaka huu pamoja na sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi, uhandisi na zingine zinazohusiana na uchumi wa bluu.
“Katika maonesha ya sabasaba Zanzibar inatangaza fursa zilizopo katika uchumi wa buluu (bahari na pembezoni mwa bahari) ambazo ni utalii, uvuvi, ukulima wa baharini, usafiri wa bahari, na tapo katika hatua ya kuendelea kutafuta wawekezaji kutoka Misri na ili kuwekeza Zanzibar. ” amesema Bw. Dunia.