……………….
NA BALTAZAR MASHAKA,MWANZA
 
TAASISI ya The Desk & Chair Foundation imetoa msaadawa vifaa vya elimu vyenye thamani ya sh.milioni 30 kwa wanafunzi 150 waliochaguliwakujiunga na masomo ya elimu ya sekondari kidato cha tano mwaka huu .

Akizungumza leo baada ya kukabidhi vifaa hivyo vya elimu,Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Dk. Alhji Sibtain Meghjee amesema msaada huo utapunguzagharama za mahitaji ya shule kwa wanafunzi hao wanaojiunga na masomo ya kidatocha tano.

“Mahitaji yote ni milioni sh.30 ambapo vifaa tulivyokwishakabidhi hadi sasa ni madaftari,mabegi mashuka,vyandarua na rim kwa wanafunzi120 kati ya 150 ambao ni nusu ya 300 walioomba,”amesema.

Dk.Alhaji Sibtain amesema wastani wa mahitaji kwa kila mtotoni sh. 650,000 lakini wamewapatia vifaa vya thamani ya sh.200,000 ilikuwapunguzia mzigo wa gharama za kununua mahitaji hasa wa familia zisizo nauwezo.

“Changamoto maombi ni mengi kuzidi bajeti iliyotolewa nawafadhili, rai yangu serikali ione namna ya kupunguza baadhi ya vifaa ili kuwapunguziamzigo wazazi ili kuwapa fursa watoto wanaochaguliwa kujiunga na masomo yakidato cha tano kumudu gharama za mahitaji,”amesema.

Kwa upande wake Mmoja wa wanufaika wa msaada huo wa vifaavilivyotolewa na The Desk And Chair Foundation,Lucia Joseph ameishukuru taasisihiyo kwa kuwasaidia vifaa mbalimbali vya elimu huku akiahidi kufanya vizurikatika masomo na mitihani yake ya mwisho.

“Binafsi familia yangu haina uwezo kutokana na kipato dunikiasi kwamba sikuwa na uhakika wa kwenda shule licha ya kuchaguliwa kuendeleana masomo ya kidato cha tano, vifaa ni vingi ambavyo hesabu yake ni zaidi ya sh.600,000.Naishukurutaasisi hii kwa kubeba sehemu ya jukumu la wazazi,”amesema.

Mwanafunzi huyo ameiomba serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kuangalia upya mahitaji ya shule kwa wanafunzi wa kidatocha tano kwa sababu ya gharama ya vifaa iko juu kiasi kwamba watoto wa familiaduni ni vigumu kuendelea na masomo.

Aidha baadhi ya wazazi wamesema shule nyingi zimeagizakila mtoto  kwenda rimu mbili za karatasiza A4,jembe,panga,kwaja (fyekeo) dawa na brusha za chooni, fagio na kuhojivifaa hivyo vinapelekwa na watoto kila mwaka vinapelekwa wapi?

“Hapa serikali inapaswa kufanya uchuguzi na ukaguzi wa vifaawanavyotakiwa wanafunzi kwenda navyo siku ya kuripoti shuleni vipo ama nibiashara ya wakuu wa shule maana haiwezekani kila mwaka mtoto anakwenda najembe,rimu,panga, fyeo na reki ,”amesema Moses Masau.

Mzazi mwingine James Masambu amesema uchunguzi alioufanyaalibaini rimu za karatasi za A4 zina soko,zinazotumika ni chache nyingizinarudi kuuzwa mitaani kadhalika majembe, mapanga,mafyekeo na dawa za chooni,nibiashara inafanywa na wakuu wa shule mtoto asipokwenda navyo hapokelewi.

“Serikali inatoa elimu bure lakini walimu wanaifanyaelimu hiyo ionekane inagharamiwa na vifaa kwa manufaa yao.Tunamwomba wazirimwenye dhamana alitolee tamko vinginevyo wananchi wataona elimu bure ni ulaghaiwa siasa,”amesema