Gabriel Jesus akishangilia baada ya kuifungia Manchester City mabao matatu dakika za 34, 50 na 54 katika ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji, Dinamo Zagreb kwenye mchezo wa Kundi C Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Maksimir, Zagreb. Bao la nne la Man City lilifungwa na Phil Foden dakika ya 84, wakati la Dinamo Zagreb lilifungwa na Daniel Olmo dakika ya 10. Manchester City imeongoza kundi hilo kwa pointi zake 14, ikifuatiwa na Atalanta iliyomaliza na pointi saba baada ya kuwafunga wenyeji Shakhtar Donetsk 3-0 jana na zote zinafuzu hatua ya 16 Bora PICHA ZAIDI SOMA HAPA
GABRIEL JESUS APIGA HAT TRICK, MAN CITY YAICHAPA 4-1 DINAMO ZAGREB
By Alex Sonna
December 12, 2019 | 4:44 am

Related Stories
View all
Michezo
2 days ago
OLBALBAL MWAMBA WA LUSAKA RHINO CUP
Mashindano ya Rhino Cup yamefikia tamati leo tarehe 8 oktoba, 2026 kwa timu ya kata ya Olbalbal kuicharaza bila huruma jumla ya Goli 3-2…
Michezo
2 days ago
KOMBE LA EPL KUTUA TANZANIA, GUINNESS KUWAPA MASHABIKI FURSA YA KULISHUHUDIA
Mashabiki wa Ligi Kuu ya England nchini Tanzania wanajiandaa kushuhudia tukio la kipekee baada ya Kombe la Ligi hiyo kutua rasmi nchini kwa mara…
