Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akifungua kongamano la 14 la Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari za Serikali za zisizo za Serikali linalofanyika kwa siku tatu Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu OR-TAMISEMI Gerald Mweli akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua kongamano la 14 la Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari za Serikali za zisizo za Serikali linalofanyika kwa siku tatu Jijini Dodoma.
Rais wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari za Serikali za zisizo za Serikali Vitalis Kulindwa Shija akielezea madhumuni ya Kongamano la TAHOSSA wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo uliofanyika mapema leo kwenye ukumbi wa mipango Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo(katikati) akisoma Jarida la TAHOSSA wakati wa ufunguzi wa Kongamano la TAHOSSA uliofanyika katia Chuo cha Mipango Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu (E) OR-TAMISEMI Gerald Mweli na Kulia ni Rais wa TAHOSSA Vitalis Kulindwa Shija.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akikabidhi zawadi kwa mmoja wa Wakuu wa shule zilizofanya vizuri katika Mtihani wa Kidato cha Sita mwaka 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akipokea Kombe la washindi wa kwanza wa Kopa Coca Coca Africa toka kwa wanafunzi walioshiriki katika amshindano hayo.
Baadhi ya wakuu wa shule wakifuatilia ufunguzi wa Kongamano la 14 la Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari za Serikali za zisizo za Serikali linalofanyika kwa siku tatu Jijini Dodoma.
…………………..
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Katika miaka minne ya utekelezaji wa mpango wa Elimu Msingi bila malipo huwezi kutaja mafanikio ya Elimu Nchini bila kuwataja wakuu wa shule ambao ndio chachu ya mafaniko ya haya katika Sekta ya Elimu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo alipokuwa akifungua kongamano la 14 la umoja wa wakuu wa shule za Sekondari Tanzania linalofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa chuo cha mipango Jijini Dodoma.
“Tangu mpango wa Elimu Msingi bila Malipo uanze Januari, 2016 Serikali imetoa jumla ya shilingi 937,548,685,734 kugharamia Elimu ya watoto wetu na katika Bajeti ya mwaka 2019/20 Serikali imetenga bajeti ya shilingi 288,485,000,000 na mpango huu umefanikisha ongezeko la watoto wanaoandikishwa kuanza darasa la kwanza, idari ya watoto wanaohitimu na hata ufaulu umeongeza kupitia mpango hii” alisema Jafo.
Serikali imepeleka fedha nyingi lakini bado jukumu kubwa lilibaki kwa Wakuu wa shule kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika ipasavyo kwa mujibu wa maelekezo na kuleta mafanikio chanya katika mpango hakika siwezi kuzungumzia mafaniko ya Elimu bila kutaja mchango wenu mmejituma kikamilifu nawapongeza sana na naomba mzidi kuchapa kazi alisisitiza Jafo.
Wakati huo huo Waziri Jafo aliwataka Wakuu hao wa shule kuhakikisha wanasimamia nidhamu kwa walimu na wanafunzi ili kujenga msingi bora wa wa utoaji na upatikanaji wa Elimu Nchini.
“Nataka mkasimamie Nidhamu mashuleni kuna baadhi ya walimu hawana nidhanu wanawatendea wanafunzi vibaya wanathubutu hata kuwapa wanafunzi ujauzito hili nataka mkalikemee, mkalisimimie na liishe katika katika shule zetu nataka kuona na kusikia walimu wote wana maadili mema na wanakuza ujuzi na ufahamu wa wanafunzi wetu katika njia iliyo bora” alisema Jafo.
Aliongeza kuwa eneo linguine ambavyo nahitaji mkaongeze usimamizi ni utoro mashuleni na hii ni kwa walimu na wanafunzi tabia hii chafu inachangia katika kurudisha nyuma jitihada za utoaji wa Elimu bora Nchini; Unakuta mwalimu hahudhurii shuleni ipasavyo, hafundishi vipindi vyake alivyopangiwa ipasavyo anafundisha vichache sababu muda mwingi hakuwepo shuleni na mwanafunzi anakosa uelewa wa kutosha wa somo husika kutokana na utoro wa mwalimu.
Na upande wa mwanafunzi hafiki shule kwa wakati au anaondoka kabla masomo hayajaisha au huenda hafiki shuleni kwa siku zote zinazotakiwa ni wazi kuwa masomo yatampita na hawezi kuwa sawa na wenzake ambao wameshiriki kikamilifu katika vipindi vyote hivi tabia hizi kwa pande zote nataka mkazikomeshe ziishe kabisa kila mwalimu na mwanafunzi watimize wajibu wao ipasavyo alisisitiza Jafo.
Waziri Jafo alimalizia kwa kuahidi panapo majaaliwa atahakikisha kuwa kikao cha mwaka2020 kinahusisha Wakuu wote wa shule za Msingi na Sekondari za Serikali na binafsi na wote watakutana kwa muda wa siku tatu na yeye atakuwa na siku maalumu ya kuzungumza na walimu wote kwa ujumla wao.
Naye Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu OR-TAMISEMI Gerald Mweli amesema kuwa lengo la kokangamo hili ni kuwakutanisha wakuu wa shule za Sekondari za Serikali na zisizo za Serikali nchini ili waweze kujifunza, kubadilishana uzoefu na kujadili kwa panoja changamoto wanazokutana nazo katika maeneo ya shule na kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja.
“Jukwaa hili ni muhimu sana kwetu kama Serikali kwa kuwa tunapata sehemu ya kutoa maelekezo muhimu ya Elimu kwa Wakuu wa shule yaan hapa ujumbe hauchakachuliwi unamfikia moja kwa moja kwa muhisika hivyo unamfikia mlengwa kama tulivyoukusudia” alisema Mweli.
Naye Rais wa umoja wa wakuu wa shule za Sekondari za Serikali na zisizo za Serikali Vitalis Kulindwa Shija amesema umoja huo una wajumbe takribani 5,000 na ulianza mwaka 2014 na hili ni kongamano la 14 kufanyika tangu kuanzishwa kwa umoja huo.
“Mpaka sasa walimu ambao wameshafika katika kongamano hili ni zaidi ya 3500 na imekua ni sehemu nzuri kwetu kukutana, kujifunza, kuwasilisha changamoto zetu na kukutana na viongozi wetu ambao imekuwa ni vigumu kukutana nao katika maeneo yetu ya kazi” alisema Shija.
Aida Rais huyo wa TAHOSSA ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuwezesha mpango wa Elimumsingi bila malipo , upatikanaji wa vifaa vya kujifunza na kufundishia, upatikanaji wa posho za madaraka kwa Wakuu wa shule na waratibu wa elimu kata na ukarabati wa miundombinu ya shule.