Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika akifungua Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma leo.
Baadhi ya viongozi wa Taasisi mbalimbali za Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika wakati akifungua Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma leo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa umma katika Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika akiteta jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa kabla ya ufunguzi wa Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma leo. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Ikulu Dkt. Moses Kusiluka.
Mwakilishi kutoka Shirika la Mendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Paul Wilson Mlemya akizungumza wakati wa Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma leo.
Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma, Mhe. Jaji (Mst.) Harold R. Nsekela akizungumza wakati wa Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (katikati mstari wa mbele) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (wa tatu kutoka kulia mstari wa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Taasisi za Umma, baada ya ufunguzi wa Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma leo.
……………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Viongozi wa Umma nchini wametakiwa kusimamia Sheria,kanuni,taratibu na miongozo ya utumishi ili kutekeleza adhima ya Serikali ya kuboresha utumishi wa Umma.
kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kepteni Mstaafu George Mkuchika wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku ya maadili na haki za bianadamu kitaifa jijini Dodoma ambapo amewataka watumishi wa Umma kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili.
“Tunaona Maadili ndio neno la Msingi,Miongoni Mwa jitihada za serikali ni kutunga sheria na kanuni mbalimbali zinazozingatia Maadili na Kanuni za utumishi wa umma,hivyo niwaase watumishi wa umma kuzingatia katika kufuata na kusimamia sheria na Miongozo ya utumumishi kwa lengo la kuboresha utawala bora”amesema.
Aidha ,amesema baadhi ya taasisi za umma zimeanzisha mabaraza ya kushughulikia utawala bora lengo kuu ni kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora.
Katika hatua nyingine Kaptain Mkuchika amesema suala la mfumo wa Mtandao limekuwa na mchango mkubwa katika kuhakiki watumishi feki pamoja na uadiluifu wa matumizi ya fedha za umma.
Awali akizungumza katika maadhimisho hayo ,Naibu Waziri ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mary Mwanjelwa amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejikita katika masuala ya uadilifiu na uzalendo hivyo kila mmoja anapaswa mambo yasiyofaa katika taifa.\
“Sisi tunatakiwa kuwa mfano bora katika kusimamia uadilifu na utawala bora hivyo niwaase watumishi wa umma kuwa jambo la uadilifu ni jambo la muhimu sana”
Kwa upande wake Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma Jaji Nstaafu Haroid Nsekela ameelezea chimbuko la siku hiyo kuwa ni siku ya kimataifa ya kuzuia na kupambana na Rushwa ambayo huazimishwa Desemba 09 ya kila mwaka
Tangu mwaka 2017 maadhimisho ya siku ya maadili na haki za bianadamu kitaifa yamekuwa yakifanyika Jijini Dodoma kufuatia maamuzi ya Serikali kuhamishia makao makuu jijini hapa na kauli mbiu kwa mwaka huu ni “maadili katika utumishi wa Umma ni nguzo Muhimu katika kuimarisha utawala bora na Haki za Binadamu”