WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene,akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Idara ya Uwekezaji Sekta Binafsi Bw.Aristides Mbwasi mara baada ya kutembelea Banda la Ofisi ya Rais,Mipango na Uwekezaji wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene,akifurahia jambo na Mkurugenzi Idara ya Uwekezaji Sekta Binafsi Bw.Aristides Mbwasi baada ya kupata maelezo katika Banda la Ofisi ya Rais,Mipango na Uwekezaji wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
Viongozi mbalimbali wa Serikali wametembelea Banda la Ofisi ya Rais,Mipango na Uwekezaji kwenye maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo yanafanyika kitaifa jijini Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 23 June, 2024.
Miongoni mwa viongozi waliotembelea ni Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene.