Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene, akizungumza leo Juni 19,2024 , wakati akifungua wiki ya maadhimisho ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinagali Park jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabiri Shekimweri,akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya maadhimisho ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinagali Park jijini Dodoma.
Na Gideon Gregory, Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amewataka wananchi kutumia simu zao kwaajili ya kufuatilia masuala ya Kiserikali na kuachana na masuala yasiyokuwa na msingi.
Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo leo Juni 19,2024 Jijini Dodoma, wakati akifungua wiki ya maadhimisho ya Utumishi wa Umma na kuwataka watumishi wa Umma kutumia wiki hiyo kupata maoni kutoka kwa wananchi wanaowahudumia.
“Ni muhimu sana wananchi wetu pia kuhamka na kuwa wafuatiliaji wa teknolojia za mifumo ya mawasiliano isihishie tu kukaa na simu kubwa, lakini simu yako sio tu kwaajili ya kutuma meseji za kawaida Whatsapp na kuangalia vitu vitu vya kawaida na baadala yake tutumie simu zetu zile zipo huduma nyingi tunaweza kuzipata za kijamii zinazotolewa na Serikali”, amesema.
Aidha amewaelekeza watendaji wote kuhakikisha Watumishi wote ambao hawajisajili kwenye mfumo wa utendaji kazi wawe wamefanya hivo kwasababu baada ya wiki hii kila mtumishi katika utumishi wa umma anapaswa kuwa amesajiliwa ili jambo hilo liweze kufungwa.
“Nafahamu kwamba kumekuwa na changamoto ya wale Watumishi ambao wako masomoni maelekezo yametolewa na katibh mkuu Utumishi nini cha kufanya, kwasababu unapokuwa masomoni unapoingia kwenye mfumo lazima huanze kuona unafanya kazi kuanzia siku umeingia kwenye mfumo, kwahiyo ukiwa huko sio lahisi kufanya kazi”, amesema.
Pia ameongeza kuwa watendaji na watumishi wa umma wanapaswa kutumia mifumo ya TEHAMA iliyobuniwa na Serikali ili kurahisisha utendaji kazi na kuepusha malalamiko kwa watumishi.
“Lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa huduma tunazozitoa zinasogea karibu zaidi na mpokea huduma ambapo ni pamoja na mwananchi yule wa kawaida.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabiri Shekimweri amesema wanaunga mkono kauli mbiu ya mwaka huu inayosema “Kuwezesha Utumishi wa Umma uliojikita kwa umma wa Afrika ya karne ya 21 iliyojumuishi na inayostawi, ni safari ya mafunzo na mabadiliko ya kiteknolojia” kwani kila mabanda yaliyopo kwenye maonesho hayo yamefungwa teknolojia mbalimbali hivyo serikali ya awamu ya Sita imelifanyia hilo kwa ufanisi zaidi.
“Hivyo niendelee kuwaarika wana Dodoma wajitahidi kujitokeza kwa wingi katika maoneshk hayo na kuweza kujifunza vitu mbalimbali pamoja na matukio mengine yanayokuja kama mapokezi ya mwenge wa Uhuru na uchaguzi wa serikali za mitaa unao kuja”,amesema.
Wiki ya Utumishi wa Umma ilianza Juni 16,2024 na itakamilika Juni 23 mwaka huu na kitika viwanja vya Chinangari Park Jijini Dodoma.