Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi tuzo Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Prof. Mark Mwandosya baada ya EWURA kuibuka kinara kati ya taasisi za Serikali zilizotoa mchango mkubwa na kwa wakati kwa Serikali katika hafla iliyofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni 2024. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt James Mwainyekule akishuhudia upokeaji wa tuzo hiyo.
Pia, EWURA ilitambuliwa kwa kuwa mchangiaji wa mara kwa mara huku ikiendelea kujiimarisha mwaka hadi mwaka .
Mchango uliotolewa na EWURA ni 15% ya mapato yote ghafi ya Mamlaka, ambayo huwasilishwa Serikalini kila mwaka kwa mujibu wa sheria ya uendeshaji taasisi za umma nchini.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Prof Mark Mwandosya(kushoto) akiteta na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ( katikati) kabla ya kupokea tuzo ya EWURA kwa kuibuka mchangiaji bora wa 15% kwa Serikali, wakati wa hafla iliyofanyika tar 11 Juni 2024, Ikulu, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile Mwainyekule.