Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde ametoa rai kwa Viongozi wa Dini kuendelea kuliombea Taifa Tanzania kushamiri katika umoja,mshikamano na Upendo na pia kuiombea serikali chini ya Mh Rais Dr John Pombe Magufuli katika kutimiza wajibu wake wa kuwaletea wananchi maendeleo.
Mbunge Mavunde ameyasema hayo jana wakati wa Uzinduzi ya Albamu ya Qaswida ya MANAAZIL ATQIYAAI ISLAMIC SOCIETY katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma,ambapo aliiomba jamii ya viongozi wa Dini kuwa mstari mbele kuhakikisha misingi ya Taifa Tanzania haivunjwi na Tanzania inaendelea kuwa moja yenye Amani,Upendo na Umoja
Wakati huo huo,Mbunge Mavunde alinunua Albamu hiyo ya Qaswida Bayana kwa kiasi cha Tsh 1,000,000 na pia kuwaahidi kupata kiwanja cha kujenga majengo ya kudumu kwa ya Taasisi yao.