Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) Selemani Jafo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake jijini Dodoma wakati akitangaza uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2020 Tanzania bara.
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa nchi ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Suleiman jafo ametangaza idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2020,ni laki 7 elfu 1na 38,sawa na asilimia 92.27.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ,Waziri jafo amefafanua kuwa miongoni mwa wanafunzi hao,wavulana ni laki 3 na 35 elfu na mia 5 na 13 sawa na asilimia 47.86 na wasichana ni laki 3 na 65 elfu na 525 sawa na asilimia 52.14.
Aidha,amesema kati ya wanafunzi waliochaguliwa ,wanafunzi 3145 sawa na asilimia 0.41 ya waliofaulu wamechaguliwa kujiunga na bweni,ambapo wanafunzi 970 watajiunga na shule ya vipaji maalum,huku 1095 watajiunga na shule za ufundi na 1080 watajiunga na shule za bweni za kawaida.
Hata hivyo,wanafunzi laki 6 na 97 elfu mia 893 sawa na asilimia 99.59 wakiwemo wavulana laki 3 na 61 elfu 866 na wasichana laki 3 95 elfu mia 6 92 wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari za kutwa katika kata mbalimbali nchini.
Katika mikoa 13 ya Tanzania bara ,ikiwemo Dodoma, shinyanga, Geita,Kagera,Katavi,Kilimanjaro,Morogoro,Mtwara,Njombe,Ruvuma, Singida,Ruvuma na Mwanza imeweza kuchagua wanafunzi wote waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza.
Licha ya hivyo jumla ya wanafunzi 58,699 sawa na asilimia 7.73 wakiwemo wavulana 28,567,sawa na asilimia 48.53 na wasichana 30,132 sawa na asilimia 51.33 ya waliuofaulu hawakupata nafasi ya kuchaguliwa kutokana na uhaba wa Madarasa.
Mikoa yenye uhaba wa vyumba vya madarasa na idadi ya wanafunzi waliobaki ni Arusha,(4739)dar-es Salaam(5808) Iringa(3480) kigoma (12092) Lindi (1695) Manyara (728) Mara (9493) Mbeya (2716) Pwani (2918) Rukwa (686) Simiyu (6616) Songwe(4684) na Tanga ni (3044).
Kufuatia hilo amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya zilizobakiza wanafunzi kukamilisha ujenzi wa madarasa ifikapo febuary 29 mwaka 2020 na kuhakikisha wanafunzi wote waliobaki wanajiounga na kidato cha kwanza ifikapo tarehe 2 march mwaka 2020.